Nimeingiwa na hofu kufuatia wizi wa madirisha site

Udochi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
787
Reaction score
1,056
Wakuu, site yangu ipo pembeni kabisa ya mji, ambako makazi ya watu ni scattered (mji mpya).

wiki Mbili zilizopita, jirani mmoja ameng'olewa madirisha mawili ya grill ambayo yana siku nne tangu yawekwe.

Juzi jirani mwingine amevunjiwa mlango usiku na kuibiwa vifaa vichache vya ujenzi vilivyobakia.

Mimi nipo hatua ya kuweka madirisha na milango, ila nina hofu kubwa moyoni, nahofia wakiniibia, ikizingatiwa nimezichanga kwa muda mrefu sana kupata hayo madirisha.

Wakuu, mnakabiliana vipi na wizi wa madirisha na milango katika site ambazo ziko pembezoni?
 
Pembezoni ipi unayoongelea? Funguka ili upate maelekezo sahihi
 
Hakikisha unaweka mlinzi kwa siku 4 baada ya kuweka grill maana kipindi hiko cement inakua haijajishikilia vizuri ,pia hakikisha fundi anapoyaweka anatindua ukuta ipasavyo kuna wengine wanaweka juu juu inakua rahisi kuyang'oa.
 
Mimi nipo hatua ya kuweka madirisha na milango, ila nina hofu kubwa moyoni, nahofia wakiniibia, ikizingatiwa nimezichanga kwa muda mrefu sana kupata hayo madirisha.
  • Hiyo fedha ifanye kazi yake; Nunua hayo madirisha na milango.
  • Kisha hifadhi na endelea na hatua zingine.
Vyote vitafungwa wakati muafaka ukifika.
 
Back
Top Bottom