Nimeingizwa kwenye kesi isiyonihusu

Nimeingizwa kwenye kesi isiyonihusu

nkolaniwe

Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
24
Reaction score
1
Ndugu wanajamvi naombeni msaada wenu,

Mimi ni mlinzi katika eneo letu la kazi, inasadikika kulitendeka wizi jambo la kushangaza lindo hilo lina zaidi ya walinzi 13.

Baada ya mpelelezi wa kituo cha polisi Kilwa Road kufika eneo la tukio aliuomba uongozi wa walinzi kupeleka jumla ya walinzi wanne kituoni. Katika shifti hiyo ya jumla ya walinzi 13 sijui niseme ni bahati mbaya au kusudi kiongozi huyo alinichukua mimi badala ya mwenzangu aliyehitajika kituoni kati ya watu wale wanne.

Nilipofika kituoni nilimfafanulia mpelelezi huyo kwa jina anaitwa Subira Tossi kuwa mimi sio kati ya watu wale wanne aliowahitaji, alichokijibu ni kuwa kama umeleta huyu basi shifti nzima ya watu 13 iletwe kituoni.

Kiongozi yule hakufanya hivyo mpaka kesi inapelekwa mahakamani tulichukuliwa watu watano yaani wale wanne na mimi niliyepelekwa kimakosa.

Tafadhali msaada wenu ili niweze kujua haki ya msingi ipo wapi au hapa kuna mazingira ya rushwa?
 
kama wewe umepelekwa kimakosa inamaana jina lako haliko katika hati ya mashtaka itakayo somwa kesi yenu ikiitwa kwa ajiri kutajwa. hivyo basi mkifika lazima mtaitwa majina na wewe utasema huusiki na kesi hii kwa kuwa haupo katika hati ya mashtaka. lakini kama jinalako lipo kwenye hati ya mashtaka basi utaeleza hayo wakati wa utetezi. hata ivyo unaweza kutoa taarifa kwa mahakama kuwa unakusudia kuweka pingamizi kuwa mshtakiwa aliyeshtakiwa siyo sahii.hata ivyo hii
 
Ukienda pale Mwembechai ukataja hilo jina la Tossi wanaweza wakakushambulia kwa mawe
 
jina langu kwenye hati ya mashitaka lipo tena n mshitakiwa namba 2 na kesi tayari ishatajwa msaada n namna gani nitaweka pingamizi katika kesi hii mahakamani.
 
Ndugu wanajamvi naombeni msaada wenu,

Mimi ni mlinzi katika eneo letu la kazi, inasadikika kulitendeka wizi jambo la kushangaza lindo hilo lina zaidi ya walinzi 13.

Baada ya mpelelezi wa kituo cha polisi Kilwa Road kufika eneo la tukio aliuomba uongozi wa walinzi kupeleka jumla ya walinzi wanne kituoni. Katika shifti hiyo ya jumla ya walinzi 13 sijui niseme ni bahati mbaya au kusudi kiongozi huyo alinichukua mimi badala ya mwenzangu aliyehitajika kituoni kati ya watu wale wanne.

Nilipofika kituoni nilimfafanulia mpelelezi huyo kwa jina anaitwa Subira Tossi kuwa mimi sio kati ya watu wale wanne aliowahitaji, alichokijibu ni kuwa kama umeleta huyu basi shifti nzima ya watu 13 iletwe kituoni.

Kiongozi yule hakufanya hivyo mpaka kesi inapelekwa mahakamani tulichukuliwa watu watano yaani wale wanne na mimi niliyepelekwa kimakosa.

Tafadhali msaada wenu ili niweze kujua haki ya msingi ipo wapi au hapa kuna mazingira ya rushwa?

Hujaeleweka vizuri..katika ilikuwaje mpelelezi akaomba apelekewe jumla ya watu wanne? kwa nini si watano? unaposema wewe si kati ya wale aliowahitaji mpelelezi unamaanisha mpelelezi huyo aliwataja watu aliowahitaji kwa majina?

Sasa iko hivi:
kama mawaazo yangu ni sahihi basi mpelelezi alipochunguza aliona jumla ya walinzi wanne waliokuwa kwenye eneo flani maalum siku ya tukio ndo wana uwezekano wa kushiriki katika tukio.

kama ni sahihi na wewe hukuwa katika eneo hilo basi tayari una utetezi wa kutosha na shahidi wako namba moja ni mpelelezi (katika kesi itabidi umhoji maagizo aliyotoa) na shahidi namba mbili ni kiongozi (utamhoji maagizo aliyopewa na mpelelezi ni kumpelekea watu gani/waliokuwa maeneo gani siku ya tukio na aliyatimizaje hayo maelezo) hapo kitendo bila kuchelewa muombe hakimu akufutie kesi kwa sababu we umechanganywa na watuhumiwa kimakosa na mwambie muheshimiwa kuwa inaonekana wewe umeingizwa katika nafasi ya mtu ambaye kiongozi wako ana mpango wa kumlinda na in that case kiongozi wako yupo katika nafasi nzuri ya kuisaidia polisi

na kabla hata hujafika huko muombe mpelelezi amjumuishe kiongozi wako katika watuhumiwa maana inaonekana ishu anaijua na wahusika anawajua ndio maana anamlinda mhusika mmojawapo.

natumaini mkiingia lindo mnasaini kitabu cha muda na maeneo mliyopangiwa kwa siku husika
 
ndugu cpt nemo umesomeka ila ni kwamba baada ya kuchukuliwa maelezo na mpelezi aliyepewa jukumu la kufungua jalada ktk maelezo yangu nilionekana kulitaja sana jina la mshtakiwa aliyetakiwa kuletwa kituoni badala yangu kwani mm na yy tulikwa walinzi wa kutumia mbwa shift hiyo ila location tofauti naye pia alijumuishwa kwenye kesi hiyo ila jambo la kushangaza mimi sikuenguliwa tena kwenye kesi hiyo mpaka kesi inapelekwa mahakamani.
 
Back
Top Bottom