mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,904
- 8,371
WASOMI WAKISHAANZA KUKOSOA UTAWALA NI HATARI KUBWA:-
Na Thadei Ole Mushi
Wasomi Nguli nchini wameendelea kuongea, wameendelea kukosoa Mkataba wa Bandari, Ukiona wasomi kaliba ya kina Shivji wameanza kutoka Vyumbani mwao na kuja kufanya Press fahamu kuwa wakati umefika wa aidha ukubali kubadilika au ubadilishwe kwa Nguvu.
Ipo hivi
Serikali yoyote dalili zake za kuondoka kwa kutokuchaguliwa kwa Kura au kwa kupinduliwa hupitia vipindi viwili muhimu:-
Normal- Ni hatua ya kwanza ni kuona mambo yapo sawa wakati hayapo sawa. Pamoja na Kelele za wananchi watawala hujiona wapo tu sawa. Mfalme Luise wa XVI na mkewe Marine Antoniete pamoja na kelele za Wafaransa kulalamika maisha magumu na kupinga hali ya matabaka (Nobles na Clerks) ambao walikuwa wakila na kusaza na mfalme, Louise aliwapuuza.
Criticism- Hii ni hatua ya pili ambayo huusisha intelectuals kama hawa kina Shivji na wengineo kuanza kupinga aidha kwa kuandika au kwa kusema waziwazi. Kipindi hiki wasomi huamua kuanika uovu na uchafu wa watawala aidha husaidia sana kuwafungua macho na akili tabaka la wasiosoma ambao ni wengi kwa kila jamii Duniani.
Wakati wa mapinduzi ya mara kwa mara kule ulaya miaka ya 1750's na kuendelea ndicho kipindi walichokibatiza kuwa ni kipindi cha enlightenment. Walijitokeza wasomi waliokuwa wanazungumza waziwazi uovu wa viongozi.
Ukiona kwenye utawala wako hizi hatua zote zinakwenda kwa pamoja jua kuna ualakini mbele. Mapinduzi yote duniani huanza na hizi hatua Mbili muhimu sana.
Kosa kubwa la watawala katika kipindi hiki ni kutumia nguvu kunyamazisha wanaopiga kelele. Matumizi makubwa ya askari hutokea kipindi hiki.
Askari katika kipindi hiki huwa watiifu kweli kwa anayewaagiza ila mbele kidogo hugeuka. Tuliona Tunisia wakigeuka na kuungana na wananchi, tuliona Zimbabwe wakati Mugabe akifurushwa askari wakigeuka na kuungana na wananchi huku wakipiga Selfie pamoja na wananchi, tuliona Misri Mubarak akifukuzwa na wananchi huku askari wakiwa pamoja na wananchi kwenye vifaru vya jeshi nk.
Nini Maoni yangu…..
Ni wakati sasa wa kuachana na Chawa kama hawa kina Kitenge, Zembwela, na wengineo kuisemea Serikali kwenye mambo ya Msingi kama haya ya Bandari. Tanzania imeshabadilika mno na kwa sasa kila mtu anaelewa….
Tanzania kwa Sasa Wasomi ni wengi sana, wapo huko mtaani wengine wanauza Juice, Wengine wanaendesha Boda Boda nk. Katika kipindi taifa linapofikia Level ya kuwa na wasomi wengi kiasi hicho viongozi wanapaswa kusoma mchezo na kuwa wajanja haswa katika kauli zao wanazozitoa, hotuba zao, taarifa zao na namna wanavyoishi nao, nk.
Nafikiri umekuwa ukiona siku za karibuni kuanzia miaka ya 2000 criticism kwa viongozi wetu zikiongezeka, Kiongozi anatoa kauli hazitapita Dk tano Atajibiwa kwa ufasaha na utaalamu uliosheheni na kauli yake inakosa maana kabisa. Hiki ni kipindi kigumu sana kwao haya ndio matokeo na Kiashiria cha kuwa na wasomi wengi nchini.
Niliwahi kusema watanzania aliongoza Nyerere sio alioongoza Mwinyi na alioongoza Mwinyi sio alioongoza Mkapa na watanzania alioongoza Mkapa sio alioongoza Jk na Wa Jk sio wale wa JPM na wa JPM sio hawa wa SSH. Kila mtu anaongoza watu tofauti na mazingira tofauti.
Kipindi Cha Nyerere kulikuwa hakuna matumizi haya ya internet leo ukisema kitu utakumbushwa Kesho kwa vielelezo.
Tanzania imeshaingia age of Enlightenment, age of reasoning ni vizuri viongozi wetu wakalifahamu hilo. Ni kazi kubwa sana kuongoza watu wa aina hiyo inahitaji uwe unaongeza maarifa kila Siku, uwe na uhusiano nao mzuri, uwasikilize na Uwe umezungukwa na watu wenye akili ndio maana huwa nasema Akili kubwa ni Mali ya Rais anapaswa kuzitumia. Badala yake tumeruhusu Rais kuzungukwa na Hizi Chawa lengo lake sijajua ni nn au ndio kumhujumu Mkuu wa Nchi.
UKOMO WA CCM
Ukomo wa Chama changu siuoni mbali, upo karibu sana kwa aina ya vijana tunaowa recruit na kuwaingiza kwenye Chama. Kama kwa Sasa tuna wananchi wanaoweza kufikiri hivi itakuwaje miaka 10 ijayo? Tumewaandaje UVCCM kuja kuchukua kijiti?
Biblia Takatifu inasema katika Mithali 18:12
“Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima.”
Morning naenda kupata Supu ya Masingiri Mahali
Ole Mushi
0712702602