Nimeiona ndege ya ATCL South Africa

Mkora

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
370
Reaction score
55
Wakuu nipo hapa Oliver Tambo Airport naiona ndege ya ATCL iliyokodishwa ipo imepaki
jee tayari wamesha vunja mkataba tena au ndio maumivu ya kichwa huanza pole pole kutokana na kazi ya Fast jet
imebidi wakubali kushindwa
nina wakilisha maana kama ndege ipo huku wao wanatumia ndege gani huko Bongo
 
Serikali inadaiwa na SAA, inawezekana hiyo ndege imeshikiliwa mpaka deni litakapolipwa
 
lolote linawezekana, chezea bongo!??
 
Haya kaka hongera kwa kwenda Bondeni, tumeshajua tayari
 
Hongera kwa kuwa Oliver Tambo Airport, mengine nayo ni ya kawaida usishangae hata kukuta imepaki hata uwanja wa Bujumbura kwani ATCL inapoharibikia ndo inapaki na kusahaulika jumla, nenda viwanja vya Kigoma, Mwanza utakuta zimepaki yaani hata injini ikiingiliwa na maji basi solution ni kupaki
 
Haya kaka hongera kwa kwenda Bondeni, tumeshajua tayari

Mkuu sasa tudege chenyewe kimoja sasa wakikipaki huku hizo safari bongo itakuwaje ?
ni pm basi ili nikuletee hata ka zawadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…