Nimeisoma, Nimeielewa, Sitaipigia Kura

Nimeisoma, Nimeielewa, Sitaipigia Kura

Kura yangu ni HAPANA

Msingida jitambue! Tambua jukumu lako, Unajua kazi yako kama Mtanzania baada ya Bunge Maalum kukamilisha jukumu lake kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, Bunge hilo lilikamilisha kazi ya KATIBA INAYOPENDEKEZWA. Hatua inayofuata ni ya wananchi kuipigia kura Katiba hiyo. Kwa kuwa nawe ni Raia wa Tanzania, nawe ni miongoni mwa wananchi ambao ndiyo wenye uamuzi na kauli ya mwisho juu ya upatikanaji wa Katiba Mpya. Hivyo jiandikishe na ukapige kura muda ukifika. Ungana na Watanzania wezako wanaoitakia nchi yao mema kuipatia Katiba nzuri inayojali maslahi ya makundi yote bila kubagua.Tumia haki yako ya kikatiba.
 
Back
Top Bottom