Nimeitwa interview UDOM lakini sitaenda...

Nimeitwa interview UDOM lakini sitaenda...

Mujumba

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
853
Reaction score
306
Niliomba kazi ya human resource pale udom, nafasi ni watu 9 lakini tuliokuwa shortlisted eti ni 712, jamani hii ni shortlist kweli au wanataka tukapoteze nauli zetu then mlacha awape kazi wapare wenzie na watu wa kaskazini??? Maana asilimia karibu 70 ya watu walioitwa ni watu wa huko...kwakweli kuliko kupoteza nauli yangu bora nipanue kilimo changu cha nyanya huku kwetu kigoma....inegkuwa wameshort list hata watu 70 afadhali lakini 712 daaaah...otherwise i wish all those who are going the best of luck out there mie siendiiiii
 
Huwezi jua mkuu, still una chance kubwa ya kushinda kaka... una probability ya 0.012% kushinda
 
Niliomba kazi ya human resource pale udom, nafasi ni watu 9 lakini tuliokuwa shortlisted eti ni 712, jamani hii ni shortlist kweli au wanataka tukapoteze nauli zetu then mlacha awape kazi wapare wenzie na watu wa kaskazini??? Maana asilimia karibu 70 ya watu walioitwa ni watu wa huko...kwakweli kuliko kupoteza nauli yangu bora nipanue kilimo changu cha nyanya huku kwetu kigoma....inegkuwa wameshort list hata watu 70 afadhali lakini 712 daaaah...otherwise i wish all those who are going the best of luck out there mie siendiiiii

Mdau,ebu rejea tangazo la kazi Mujumba! Nafasi za hiyo kada ni 15 na siyo kama ulivyotaja,au mi ndo sijui!
 
The more people they interview, the more they get paid. Ndiyo mpango mzima.

Pia inakuwa rahisi ku-pick mtu wanayemtaka, as there is less likely to be any complaint.

Nafikiri zilikuwa nafasi 15. Kama walioitwa kwenye interview ni 712, then kila nafasi ni watu 47.

Unless mnaenda kwanza kufanya assessments kabla ya the actual interview then it is not worth it

Kwenye nchi za watu employer akiita watu wengi hivyo kwenye interview, the best candidates will not turn up for the interview.

Employer anakuwa discredited and no talent will prepare to work for such an employer.
 
Enzi hizo nilikuwa na kauli mbiu yangu,ilikuwa inasema.Kosa kubwa atakalofanya mwajiri ni kuniita katika usairi,iwe kwa njia ya mahojihano,mtihani wa kuandika au kuwasilisha mada,kwa kweli mwajiri lazima anipe kula ya turufu,Vimemo lazima vitachanwa tu.Mungu yupo daima,lakini binadamu ufa,kujaribu ni jambo jema
 
mkuu kama roho imesita usipoteze mda wako parangana na kazi zako mwanawani c nakukatisha tamaa wala nini hapo udom ni pagumu.
 
Jamani hivi hizo interview ni tarehe ngapi, coz nimeona majina bila maelezo muhimu?
 
Niliomba kazi ya human resource pale udom, nafasi ni watu 9 lakini tuliokuwa shortlisted eti ni 712, jamani hii ni shortlist kweli au wanataka tukapoteze nauli zetu then mlacha awape kazi wapare wenzie na watu wa kaskazini??? Maana asilimia karibu 70 ya watu walioitwa ni watu wa huko...kwakweli kuliko kupoteza nauli yangu bora nipanue kilimo changu cha nyanya huku kwetu kigoma....inegkuwa wameshort list hata watu 70 afadhali lakini 712 daaaah...otherwise i wish all those who are going the best of luck out there mie siendiiiii

Labda mkuu ungeeleza umejuaje kuwa watu 70 ni wapare na watu wa kaskazini kwani ku-rely kwenye saduku la posta ni void argument ambayo justification yake haitakuwa na mashiko kwani makabila yametapakaa almost nchi nzima now days
 
Hata mimi naungana na wewe, huu si utaratibu mzuri,utaitaje candidates 534 kwa vacancies 17?haya masihara kabisa, nadhani watakuwa wanatukebehi tu kwa kuzidi kutupigilia misumari kwenye vipara vya vichwa vyetu. Hali ngumu ndugu zanguni,Mbeya to Dom siyo mchezo halafu wanakuzingua.siyo mchezo mzuri kabisa huu.Walitakiwa shortilist angalau itie matumaini.Anyway all the best wadau.
 
Huna akili kabisa wewe kwa hiyo wewe aliyekupa hizo takwimu za makabila ni nani!? Mimi ninaishi moshi lakini si mpare wala sina asili ya kaskazini!!
kwa hiyo sikustahili kuitwa kwakuwa natokea huku!? kwa hiyo watu wa Kaskazini hawastaili kuitwa manake wewe wa kigoma kuitwa umeona sawa ila unalalamika eti wameitwa watu wa kaskazinyai!!
Kwanza hauna sifa za kushinda inaelekea ulisoma na Mulugo wewe ndio maana umeona namba watu ni 700 umogopa kwenda! ila kumbuka hao 15 wanatokea katika hao 700 so kama ungekuwa the best ungeenda na uwashinde hao 700 ila kwa kuwa ni kilaza unaogopa kuburuzwa kama utaenda...Usiende manake hata ukienda hautashinda hiyo interview wewe kilaza
 
me naona cjui nimo au vp maana majina mawimawili icjekua kakusudiwa mwengne nikaenda namm nikafulia, naomba mwawazo wakuu
 
Kazi kweli kweli,hapo tayari wana watu wao tayari kwa sisi tuijuao Udom,jamaa angu kaitwa System Administrator wamekua shortlisted watu 234 lakn wao wanataka watu 4 wakati yupo mtoto wa mkuu wa kitengo flani hapo Udom kimsingi sasa ni nafasi 3 tuu.
 
Jamani hivi hizo interview ni tarehe ngapi, coz nimeona majina bila maelezo muhimu?

hawako serious hawa, utwaitaje watu kwenye interview bila tarehe? wanaendelea kudhihirisha uzembe wao
 
Oooh interview leo imeanza wakuu. Mimi sio muhusika just student hapa... sina full data ila naona nyomi ya watu hapa chimwaga.
 
aliyewaambia mmeitwa ni nani? Imeandikwa wp kuwa hiyo ni 'shortlist'?...ukiwa kilaza kama Mulugo unaanza kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.... Subirini utaratibu mtapewa tu.. Msidandie train kwa mbele mtakufa buure.Hayo ni majina tu kwenye database yao!
 
Acha kukurupuka kudis vitu usivyovijua utakuja pakakatwa ww!!
Soma heading ya hayo majina unayosema yapo kwenye database yao. JIPANGEE
 
Kila mtu sasa anakula kwa urefu wa kamba yake. Usipoteze muda kaka, kama kweli hiyo ni shortlist basi achana nao. Sijawahi kusikia mahali pengine nafasi moja watu 47!, hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ipi ya utumishi?
 
Back
Top Bottom