Nimejambiwa live na wachawi leo

Mkuu,maskhara hayo mkuu.....kunusana tena!!!!Ayseee,au ndiyo ile design ya "kula tunda kimasihara" mkuu???!!!!Maana mna maskhara sana na mwenzi wako!!!!
 
Hayo mambo yapo. Siku moja nililazwa hospitali, kwa nje kulikuwa na chemba ya maji machafu. Asubuhi ya siku iliyofuata nilisikia harufu mbaya na kali sana, nikadhani inatoka kwenye ile chemba. Baada ya kuwa kuruhusiwa, nikiwa kwenye daladala, mambo yalikuwa safi. Lakini baada ya muda mchache kupita, nilisikia vitu kama baloon ndogo vikipasuka maeneo ya mbele ya uso, na ikatoka harufu ile ile kama ya kwenye zile chemba za maji machafu. Abiria waliishia kugeuka kuangalia hii harufu inatoka wapi. Kifupi ni kwamba si lazima iwe wachawi walioleta harufu hiyo, maana kuna 'nguvu' nyingine iliyo 'ovu' (nikimaanisha mashetani - satan & demons) inayoweza kufanya mambo hayo.

Cha ajabu zaidi siku ya kwanza nilipokwenda hospitali, nikiwa nakaribia kufika mapokezi, nilishangaa suruali inavuka, nilipoangalia nikakuta sina mkanda, umepotea. Nilikuja kuukuta huo mkanda kwenye mfuko wangu wa rambo asubuhi, tena mkanda umekunjwa vizuri, wakati natafuta dawa ya meno na mswaki. Hao waliofanya mambo hayo walikula kichapo kikali kutoka kwa NGUVU kubwa zaidi yao (YESU KRISTO), na wanajuta hadi sasa. Mengine kuhusu wao na walivyopigwa kipigo cha aibu siyaleti maana si majibu kwa mada husika hapo juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…