Nimejambiwa live na wachawi leo

Nimejambiwa live na wachawi leo

Habari za leo wakuu.

Wazee uchawi upo asee. Dah nipo home na wife nikasikia bonge la mjambo kubabeki sasa ishu kuanza kulalamikiana nani kajamba.
Amekimbia faster chumbani nikajua anakwepa harufu na kunikwepa mimi kumbe alikimbilia pafyumu kwa ajili ya kupulizia.

Bana wewe nikajikuta na mimi namkimbilia nijuee labda kajamba yeye maana alikuwa ananituhumu. Cha kushangaza tumeingia chumbani harufu hakuna sasa kuanza kunusana bana hakuna kitu ndio tukaanza kushangaa kurudi sebuleni harufu bado ipo ya ukweli tena ilizidi upande niliokuwa nimekaa bana.

Baada ya hapo wife akasema itakuwa harufu inatoka nje. Kutoka nje kuhakikisha labda inatokea nje hakuna kitu pako safi kabisa.

Naomba kuuliza wazoefu je ilisha wahi kumtokea mtu?

Na je wana maana gani hawa au huyu mtu na nifanye nini kukomesha hii tabia maana hii si mara moja.

Mara nyingi inatokea hali hii mpaka inazua ugomvi wa nani kajamba. Nimeshtuka sana.
Mkuu,maskhara hayo mkuu.....kunusana tena!!!!Ayseee,au ndiyo ile design ya "kula tunda kimasihara" mkuu???!!!!Maana mna maskhara sana na mwenzi wako!!!!
 
Habari za leo wakuu.

Wazee uchawi upo asee. Dah nipo home na wife nikasikia bonge la mjambo kubabeki sasa ishu kuanza kulalamikiana nani kajamba.
Amekimbia faster chumbani nikajua anakwepa harufu na kunikwepa mimi kumbe alikimbilia pafyumu kwa ajili ya kupulizia.
Hayo mambo yapo. Siku moja nililazwa hospitali, kwa nje kulikuwa na chemba ya maji machafu. Asubuhi ya siku iliyofuata nilisikia harufu mbaya na kali sana, nikadhani inatoka kwenye ile chemba. Baada ya kuwa kuruhusiwa, nikiwa kwenye daladala, mambo yalikuwa safi. Lakini baada ya muda mchache kupita, nilisikia vitu kama baloon ndogo vikipasuka maeneo ya mbele ya uso, na ikatoka harufu ile ile kama ya kwenye zile chemba za maji machafu. Abiria waliishia kugeuka kuangalia hii harufu inatoka wapi. Kifupi ni kwamba si lazima iwe wachawi walioleta harufu hiyo, maana kuna 'nguvu' nyingine iliyo 'ovu' (nikimaanisha mashetani - satan & demons) inayoweza kufanya mambo hayo.

Cha ajabu zaidi siku ya kwanza nilipokwenda hospitali, nikiwa nakaribia kufika mapokezi, nilishangaa suruali inavuka, nilipoangalia nikakuta sina mkanda, umepotea. Nilikuja kuukuta huo mkanda kwenye mfuko wangu wa rambo asubuhi, tena mkanda umekunjwa vizuri, wakati natafuta dawa ya meno na mswaki. Hao waliofanya mambo hayo walikula kichapo kikali kutoka kwa NGUVU kubwa zaidi yao (YESU KRISTO), na wanajuta hadi sasa. Mengine kuhusu wao na walivyopigwa kipigo cha aibu siyaleti maana si majibu kwa mada husika hapo juu.
 
Back
Top Bottom