Nimejaribu nimeshindwa, Sasa nimeamua kuoa!

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Mpango wangu wa kutaka mwanamke wa kihindi umegonga mwamba.
Nimejaribu kwa wanawake wanne akiwemo na yule aliyewahi kuniminya
mkono kule posta, watatu wamenikataa huku mmoja akisita kutokana
na hofu ya familia yake na kitisho cha kurudishwa India kama alivyofanyiwa
dada yake ambaye alichumbiwa na Mpemba.
Imeniuma sana maana zoezi lote hilo nimeambulia kujifunza kihindi tu
kama nilivyoshauriwa na wadau hapa jukwaani.

Kwa sasa nimepata mwanamke wa Msumbiji ambaye baba yake ni mreno (Hamjui)
mama yake ni mwafrika. Na ninakukaribisheni (angalau muhudhurie kwa roho zenu)
katika ndoa itakayofanyika Jumamosi ya Tar 29/12/ 2012 Mungu akipenda.
Ndoa itafanyika Mweda au Nangadi kutokana na makubaliano ndugu wa bi Harusi
mtarajiwa. KARIBUNI SANA.
 
Tuwekee na kapicha ka huyo shemeji yetu mkuu.
 
Duuh uncle kumbe uliikataa kabisa rangi nyeusi, umezuga na wahindi bila mafanikio sasa unachotara wa kireno. Hongera ndugu.
 
Hongera kwa kupenda rangi. Kinachofuata ni kufungua kiwanda cha mbao sofala.
 
Mwanamke wa nchumbiji raha, we nchomba utafaidi utamu. Hongera iko siku utakuwa shemeji au binamu wa christian ronaldo.
 
Duuh uncle kumbe uliikataa kabisa rangi nyeusi, umezuga na wahindi bila mafanikio sasa unachotara wa kireno. Hongera ndugu.
mimi nina chotara wa kifaransa.
Ila jamaa asiwe kapata mmakonde anamwita mreno
 
Dah umenikumbusha ile story ya mine boy yule mbinti aliyekuwa na kauli hii I'm black outside, but I'm as white as Europeans inside me.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…