Nimejenga nyumba hii kwa 4,500,000/=

wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.

Mkuu umeona yaliyotokea stendi ya Ubungo leo? Sasa ule ulikuwa uzio tu
 
Umeijenga wapi? Hebu tusaidie kwa kuweka mchanganuo na ina vyumba vingapi? Kwani kwa uzoefu wangu hiyo hela ni ya foundation tuu kwa nyumba ya kawaida kwa Dar, otherwise haitoshi hata foundation. Kiwanja je?
 
Kazi nzuri mkuu hapo hata kama haujamalizia finishing za ndani unahamia utamalizia polepole (badala ya kumlipa mwenye nyumba hizo pesa unamalizia nyumba yako)
 
Hongera sana. Hapo utakuwa umetumia matofali ya kuchoma kama sikosei.
 
HONGERA sana na hamia fasta utupunguzie idadi ya wagombania mapango(nyumba za kupanga)
 
wakuu hamuwezi amini ninejikakamua kujenga Nyumba hii kwa bei tajwa hapo juu, kumbe ki la kitu ni maamuzi tu.

Yes nakubaliana na wewe,maana bati zenyewe naona umechukua pale veterinary-tazara,hali kadhalika madirisha na mirango,pia tofadhi ni za tope,alafu inaonyesha ni rufiji sio Dar.
By the way hongera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…