Nimejenga nyumba hii kwa 4,500,000/=

Nimejenga nyumba hii kwa 4,500,000/=

umejengea wapi mkuu? kwani wengi tunahitaji kujenga nyumba kama hizo za bei rahisi, kwani sehemu nyingi hii ni bei ya kiwanja tu! hebu fanya mchanganuo basi tukuelewe mkuu
 
Kwa kweli hata mimi nashangaa sana kwa miaka hii kujenga nyumba kwa hela hiyo hizi ndoto za abunuasi jamani maana sijui na kuweka ungo yaani dish la digitali mhm! mmapo mbombo ngafu!
 
rakeyescarl upo kweli umeona mwenzio kajenga nyumba kwa shilingi 4,500,000/= si ndoto za abunuasi hizi sijui lakini inabidi atuoneshe mchanganuo wa bajeti yake nzima ya ujenzi ulipoanza na mwisho wake maana tunataka tufahamu.
 
Last edited by a moderator:
hongera mkuu,manake wengine hawatak kujenga hadi wawe na cash 20m.hapo unaweka matoleo,ukiashiria mpambano unaendelea!hongera sana

Hiyo nyumba inaonekana ina zaidi ya miaka 20, so tukiangalia time value of money , iyo pesa bado ni nyingi kipindi cha miaka 20 iliyopita hasa na location yenyewe iliyopo
 
Mkuu kama haujui kaa kimya, tofali za udongo sh 30 na wakikuchomea ni sh 50

Acha Uzushi wako wewe unajifanya unajua wakati we mwemyew hamna kitu hebu nielezee ni maeneo gani ambapo waweza pata tofali kuchomwa kwa shiling 50?
 
Mmmmmh,INAHITAJI Moyo kukuamini HASA katika zama HIZI AMBAZO vifaa vya UJENZI ni GHARAMA na Mafundi WAMEKUWA na GHARAMA kubwa,hata na hivyo HONGERA kwa kulifanikisha hili maana kwako ni kwako,na WENGI wetu tumeshindwa KUJENGA mahala pa kutusitiri.
 
umejengea wapi mkuu?
kwani wengi tunahitaji kujenga nyumba kama hizo za bei rahisi, kwani
sehemu nyingi hii ni bei ya kiwanja tu! hebu fanya mchanganuo basi
tukuelewe mkuu

Nitaweka mchanganuo mtakuja amini tu. Nimejenga mikoa ya kanda ya kati mkuu.
 
Mwenye nyumba akiweka mnyambulisho na mlinganyo wa gharama jinsi alivyo jenga hiyo nyumba kwa kiwango cha fedha alicho sema na mimi najenga yangu kesho asubuhi na mapema.
Please....mimi ni mbeba zege mzuri tu usininyime ajira!
 
Back
Top Bottom