Nimejiajiri kama Blogger, hata nawe unaweza jaribu

Nimejiajiri kama Blogger, hata nawe unaweza jaribu

Mjasiriamali M

Senior Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
142
Reaction score
69
Habari ndugu zangu, leo naomba nami niongee neno katika uwanja huu wa kijasiriamali, Mimi ni mhitimu wa Degree ya Uhasibu miaka 3 iliyopita, tangu kipindi hicho chote sijapata ajira ya kudumu na rasmi, Namshukuru Mungu niliwahi kusomea mambo ya I.T kwa level ya Certificate nilivyomaliza Form 6 mwaka 2000.

Sasa baasi, baada ya kusota miaka yote huku nikihangaika kwa hili na lile, nikapata wazo la kuwa Blogger, ingawa mwanzoni ilikuwa ngumu lakini sikuacha kujituma na kujifunza toka kwa waliofanikiwa kwani hata wao walianzia chini.

Kwa muda wa miezi sita ya mwanzo nilikosa Direction nzuri kwani kila kitu nilikuwa nataka kufanya au kuandika mimi, kuna kipindi nilikata tamaa na kuona kwamba Kupata mafanikio kupitia Blogging si kwangu mimi'

Hata hivyo kipindi hicho kigumu kilipita na nikapata kibarua fulani ambacho kilinifanya nijitume na kujikusanya katika suala zima la fedha na kuweza kununua laptop mpya na universal modem ambavyo ndio kama JEMBE na SHOKA langu.

Baada ya hapo nilijipanga kwa kuwa naandika Articles zenye kuvuta hisia za wasomaji wangu huku nikiendelea kujifunza nami kadri siku zinavyoenda. Kwa uchache nawashauri Vijana wenzangu ambao tuna access na internet na tuna muda kujifunza na kufanya hivyo kwani mimi nimeanza kuyaonja matunda ya blogging kupitia Google Adsense kwani hata leo nimetoka kuchukua Hela zangu Kupitia Western Union.

Pia binafsi nimeanzisha blog ambayo tutakuwa tunaelekezana na kufundishana mambo mbali mbali ikiwemo na mbinu za kufanya ili kufikia mbali katika blogging.

Kwa vile si mtaalamu sana wa ki teknolojia na computer science ntakuwa natoa facts ambazo hata mimi mhasibu nilizipitia na mpaka leo nami napata kidogo kupitia Google Adsense.
Tafadhali tembelea http://www.tanzaniabloggers.com tuna mengi ya kuelezana.
 
kichwa changu kigumu kuelewa, nielezee jinsi adsense inavyofanya kazi.
 
kichwa changu kigumu kuelewa, nielezee jinsi adsense inavyofanya kazi.
Usijali kaka, kama ungetembelea blog yetu ya tanzaniabloggers.com ungepata pa kuanzia maana huko tumejaribu kuelezea kwa uangalau kidogo mkuu.
 
Mjasiliamali M, Mkuu umeandika mambo yanayoelimisha sana na hasa link ulizoweka nimepata maarifa makubwa sana juu ya hii aina ya upashanaji habari na maarifa. Ni kwa mengi ninayojifunza hapa JF kama ulivyoonyesha ukarimu wako hapa ndiyo imekuwa chachu kwangu kushea na watu ninachoona kinaweza kuwafanya kesho yao ikawa bora kuliko leo. Let us keep on sharing, ukitaka kupokea toa kwanza!!
 
Mjasiliamali M, Mkuu umeandika mambo yanayoelimisha sana na hasa link ulizoweka nimepata maarifa makubwa sana juu ya hii aina ya upashanaji habari na maarifa. Ni kwa mengi ninayojifunza hapa JF kama ulivyoonyesha ukarimu wako hapa ndiyo imekuwa chachu kwangu kushea na watu ninachoona kinaweza kuwafanya kesho yao ikawa bora kuliko leo. Let us keep on sharing, ukitaka kupokea toa kwanza!!

Asante kaka, pamoja sana, kama vijana wa leo inatubidi tubadilike ili kukabili changamoto zilizopo mbele yetu. Shukrani kaka.
 
wewe ni jembe.keep it up mkuu. Mungu akufanikishe na kukuwewezesha.....keep moving..zamani nikiwa o level mwalimu wangu alinifundisha wimbo fulani wa ''ONE FINGER ONE THUMB KEEP MOVING''
 
Asanteni wakuu, naimani woote tunaweza kufikia hapa na mbali zaidi, kikubwa ni kuthubutu na kuwa tayari kujifunza zaidi.
 
ni kweli mkuu. mimi ni logo designer na asilimia 99 ya business inayohusiana na kazi zangu nafanya kupitia mtandaoni na faida ninaiona. sasa hivi nina wateja kuanzia sweden, palestina na hadi uingereza. dakika 10 tu zilizopita mteja mtarajiwa kutoka kenya kanitumia namba ya simu nimtafute tomorrow in shaa Allah. hakika, blogging inaweza kukukwamua kiuchumi
 
Hongera kwa hilo kaka, pamoja sana, kwa sekta hiyo i will surely contact you, we might work things out pamoja sana. Swaum Njema.
 
Back
Top Bottom