Nimejiajiri kama Blogger, hata nawe unaweza jaribu

Nimejiajiri kama Blogger, hata nawe unaweza jaribu

I create rhythm in design. I am Logoriddim. C'mon risen up... Reload your image. Get a logo. Now!
 
Uzi wako unaelimisha sana. Binafsi ninanufaika kwa kuwa blogger. Namshukuru sana Mwenyezingu maana kanijaalia Nafanya kazi na watu ndani na nje ya nchi. Hii ni fursa ambao inatakiwa tuitumie inatakiwa tuitumie ipasavyo

Habari ndugu zangu, leo naomba nami niongee neno katika uwanja huu wa kijasiriamali, Mimi ni mhitimu wa Degree ya Uhasibu miaka 3 iliyopita, tangu kipindi hicho chote sijapata ajira ya kudumu na rasmi, Namshukuru Mungu niliwahi kusomea mambo ya I.T kwa level ya Certificate nilivyomaliza Form 6 mwaka 2000.

Sasa baasi, baada ya kusota miaka yote huku nikihangaika kwa hili na lile, nikapata wazo la kuwa Blogger, ingawa mwanzoni ilikuwa ngumu lakini sikuacha kujituma na kujifunza toka kwa waliofanikiwa kwani hata wao walianzia chini.

Kwa muda wa miezi sita ya mwanzo nilikosa Direction nzuri kwani kila kitu nilikuwa nataka kufanya au kuandika mimi, kuna kipindi nilikata tamaa na kuona kwamba Kupata mafanikio kupitia Blogging si kwangu mimi'

Hata hivyo kipindi hicho kigumu kilipita na nikapata kibarua fulani ambacho kilinifanya nijitume na kujikusanya katika suala zima la fedha na kuweza kununua laptop mpya na universal modem ambavyo ndio kama JEMBE na SHOKA langu.

Baada ya hapo nilijipanga kwa kuwa naandika Articles zenye kuvuta hisia za wasomaji wangu huku nikiendelea kujifunza nami kadri siku zinavyoenda. Kwa uchache nawashauri Vijana wenzangu ambao tuna access na internet na tuna muda kujifunza na kufanya hivyo kwani mimi nimeanza kuyaonja matunda ya blogging kupitia Google Adsense kwani hata leo nimetoka kuchukua Hela zangu Kupitia Western Union.

Pia binafsi nimeanzisha blog ambayo tutakuwa tunaelekezana na kufundishana mambo mbali mbali ikiwemo na mbinu za kufanya ili kufikia mbali katika blogging.

Kwa vile si mtaalamu sana wa ki teknolojia na computer science ntakuwa natoa facts ambazo hata mimi mhasibu nilizipitia na mpaka leo nami napata kidogo kupitia Google Adsense.
Tafadhali tembeleaTanzania Bloggers | Mabadiliko Chanya katika Blogs Tanzania tuna mengi ya kuelezana.
 
Mkuu Nimepitia hii blog.. its very simple hata LOGO hujaweka mkuu.
Ila poa poa kazi nzuri.Unajitangaza vyema na mie nitakuta one day mkuu

Asante. Kwa sasa niko busy sana ila hivi karibuni nitaifanyia maboresho stahiki in shaa Allah
 
I create rhythm in design. I am Logoriddim. C'mon risen up... Reload your image. Get a logo. Now!

Changamkia fursa ya kufungua blog utangaze huduma/ bidhaa zako. Google blog ni bure na kwa muda mfupi ukijitangaza wadau wengi ndani na nje ya nchi watakutambua.
 
Ushauri Wa bure: hakikisha unaisajili logo/nembo yako au trade name yako pale brela. Ni gharama nafuu kiasi. Kwa kufanya hivyo utakuwa unailinda project yako dhidi ya mafisadi ambao wanaweza kutumia trademark yako kwa faida zao binafsi
 
Kwa Kila kazi moja ya kutengeneza logo utakayofanya na mimi Utapata offer ya bure ya 1. Proforma Invoice Template 2. Tax Invoice Template 3. Delivery note template 4. Headed Paper Template 5. Biz Card Template.
Contact: (mobile/whatsapp/viber): +255 688 999006
logoriddim@yahoo.com
Ili kujiridhisha juu ya uwezo wangu Tafadhali tembelea blog yangu ifuatayo: http://logoriddims.blogspot.com/
Karibuni sana.
 
Mifano ifuatayo ya baadhi ya kazi zangu ina lengo la kukuhamasisha zaidi
ImageUploadedByJamiiForums1420484210.223982.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1420484247.593975.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1420484296.806350.jpg
 
jamani naomba msaada Wa kufungua blog haraka sana

Ni rahisi sana pengine kufungua blog mkuu.Hasa hizi za blogspot.com,wordpress.com n.k..
Kikubwa ni lengo lako husika hasa upande wa content.. Kama Umejipanga hivyo basi kila la kheri.Wadau watakusaidia kufungua mkuu.Mimi sio mzoefu sana!
 
NYONGEZA YA USHAURI:-

Kwa kipindi Kirefu kiasi nimekuwa katika mambo haya ya Blogging, nimeona na kujifunza mengi, nitoe wito kwa Vijana wenzangu ambao bado hatujapata Ajira Rasmi au wale ambao tupo kwenye Ajira na Tunafikiria Wapi tunaweza kupata nafasi ya kuanzisha Biashara ama Kuwekeza, basi Angalia na Karibu katika Ulimwengu wa Blogging, Ni Zao la kipekee ambalo endapo utalilima na kulilea kwa Misingi inayotakiwa kamwe haliwezi kukutupa Ingawa Lina Changamoto Nyingi. Karibu Tujadiliane na Kupeana Njia zaidi. Kila la Kheri kwa wote watakao kuwa tayari kuthubutu.

Mabadiliko chanya, yanaanza sasa.
 
Back
Top Bottom