Nimejiajiri kama Blogger, hata nawe unaweza jaribu

Ukifikisha Euro 70 wanaanza kukulipa, ila depending na traffic katika site yako unaweza ukapata Euro 70 Hadi 300. Mimi nacheza hapo.
hongerah mkuu, tatizo la blogs ni kuwa idea inayofanana, wewe umetoka kivingine kabisaa!

umekuja na idea ya kipekee, ngoja niumize kichwa na mimi nipate idea ya kweli !
 
hongerah mkuu, tatizo la blogs ni kuwa idea inayofanana, wewe umetoka kivingine kabisaa!

umekuja na idea ya kipekee, ngoja niumize kichwa na mimi nipate idea ya kweli !
Kila la kheri mkuu, tuwasiliane incase unakwama popote
 
Bloggers Seminar/Training
Habari za Leo wapendwa Bloggers, Nimatumaini yetu Mnaendelea Vizuri na Shughuli zenu za Ujenzi wa Taifa na Zaidi ya yote ni wazima kiafya. Kama Kichwa cha habari kinavyojieleza, Team nzima ya Tanzania Bloggers imedhamiria kutoa mafunzo na majadiliano ambayo yanalenga kuwapandisha Thamani na kuwaongezea Uelewa Zaidi Bloggers wa Kitanzania ili kufanya Blogging kama Ajira na sio Kubahatisha.
Kupitia mafunzo hayo tunaimani Bloggers watapata ufahamu zaidi juu ya mambo makuu matano(5):-
1. Basic Blogging Skills
2. Nafasi ya Blogging katika Kujikwamua kiuchumi, na nini cha kufanya kuanzia hapo ulipo.
3. Ku design simple na kwa manufaa ya kujipatia kipato
4. Google Adsense, Jinsi ya Kujiunga, Faida, Masharti na Njia Nyingine Mbadala za Kupata Hela Mtandaoni.
5. Kutengeneza Umoja (Network) nzuri ya Bloggers wa Kitanzania ili kusaidiana na kUfahamishana juu ya Mambo mbali mbali huku tukipata Miongozo Toka kwa Bloggers waliofanikiwa na Technicians.

Tanzania Bloggers, Itawasaidia wale wote ambao bado hawajapa Akaunti za Google Adsense mbinu na jinsi gani watazipata Akaunti Hizo ili Kujipatia Kipato, Pia Tutawawezesha Bloggers kuwa na angalau Njia 3 Mbadala za Google Adsense katika Blog zao ili kuweka mazingira ya kupata zaidi na tahadhari ikitokea mlango mmoja umefungwa.

Kwa wale wenye Ndoto na Mawazo ya Ku Blog lakini hawana Uwezo wa Ku Design basi hii ni fursa kwao kwani Mtapata nafasi ya Ku designiwa Blogs zenu vizuri katika viwango vya kimataifa ili kujipatia kipato au kuonesha mvuto na utofauti kupitia Templates za Design tofauti tofauti na plugins nzuri zisizo load Polepole.

GHARAMA:-
1. Ikiwa ni kuja kusikiliza tu na kufunguliwa kimazo juu ya mbinu na mwenendo mzima wa Blogging, ni Tsh Elfu 5 (5,000/= Tu) Ili baada ya kusikiliza basi kila kitu utajifanyia mwenyewe.
2. Ikiwa utapenda upatiwe Elimu na kufunguliwa Blog, Kuwekewa Adsense na Matangazo mengine ambayo yatakupa kipato, Blog Designing, Face book page na Plugins nyingine Nyingi, Gharama ni Tsh Elfu Thelathini (30,000/=)
3. Ikiwa Utahitaji ufanyiwe yote hayo ya kipengele cha pili huku Blog Yako Ikisomeka kwa jina unalotaka wewe Mfano www.jinalangu.com basi gharama itakuwa Tsh Elfu Sitini (60,000/=)

Naimani hii ni Fursa kwako ewe Kijana Mwenzangu ambaye tayari una Blog au unapenda kuwa na Blog na Ujiendeshee maisha yako kupitia Nyanja hii, Ikiwa una access ya Compute na Internet basi yawezekana ikawa ndio Life Time Investment Yako kwa gharama ndogo, sawa na Bure.
Pia kwa wale ambao wapo makazini na wanalipenda hili kama hobby basi hii ni nafasi kwa hao part time bloggers.

UTARATIBU WA MALIPO:-
Asilimia Arobaini (40%) ya Malipo yatafanyika siku Tatu au Mbili Kabla ya Training na Training ziakuwa za awamu mbili, ya kwanza ni ya wadau wa tsh 5,000/= nay a pili ni ya tsh 30,000/=, ambapo mshiriki atafika katika ofisi za TanzaniaBlogers/Wanajamii na kulipia kisha kupewa stakabadhi amabayo ndio kitambulisho chake siku ya training yake , hii itasaidia kujiwekea nafasi ya kiti siku ya Tukio.
Pia Kwa wale ambao wanaweka hela kwa kudunduliza basi unaweza ukaja ofisini, ukaandikisha jina na Program ambayo inakufaa, utauwa unaleta kiasi hicho kidogo kidogo mpaka mwisho utakapokamilisha, pia ukishafika siku ya kwanza waweza tuma malipo yako kupitia simu.

SIKU na MUDA.
Juamosi ya Tarehe 31/08/2013 na Jumapili ya Tarehe 01/09/2013. Kuanzia Saa Nane Mchana Hadi saa 11 Jioni.
UKUMBI
Kulingana na Idadi ya Watu Tunatarajia kuchukua madarasa mawili katika shule za karibu na maeneo ya ofisi zetu, yaani Tandika Maghorofani karibu na Chuo cha Taifa cha Utalii na Chuo cha Bandari.

MENGINEYO
Tunatarajia Kupata japo maji/juice Depending na Idadi ya Watu hasa kwa wadau wa tsh 5,000. Malopo yaliyobaki yatafanywa siku ya Training kwa atakaependa na ambaye atakuwa hajamaliza malipo yote.

MUHIMU ZAIDI.
Tanzania Bloggers haitakuacha Ewe Blogger Ukiwa Umekwama kwa Lolote kuhusiana na Blogging Mpaka nawe uwe katika nafasi ya kunyanyua wengine zaidi.
Natanguliza Shukrani za Dhati na Nimatumaini yangu nitakuwa nimeeleweka.
Kwa maswali na lolote la ziada tafadhali tuwasiliane kupitia:-
tzbloggers@gmail.com
0752 981 380
0719 447 204.


 

Habarini za leo jamaa wote wachakarikaji. Hapa nataka kuwaonesha mafanikio yangu machache niliyopata kupitia biashara ya blogging. Mimi ni logo designer (nachora nembo) na hapa chini nakuonesha baadhi ya kazi zangu nilizofanya na wateja nje ya nchi. Aidha kwa hapa nchini, nimeshafanya kazi nyingi sana ambazo unawezakuziona kwa kutembelea blog yangu ifuatayo:LOGO DESIGNER
View attachment 114872 View attachment 114875View attachment 114876
 
Mwaka Mpya 2014 tuzitumie fursa zinazopatikana mitandaoni kuzikuza kazi/miradi yetu
 
Je, wewe umefaidika kwa kutumia mbinu hii ya mitandao kutafuta masoko. Je, una lolote la kuchangia ili kuwahamasisha watanzania wengine?
 
Namshukuru Mwenyezimungu... Bado ninanufaika kikazi kwa kuwa blogger. Nawe pia jaribu kutumia fursa hizi za utandawazi kwa ajili ya manufaa yk na ya taifa kwa ujumla
 
Mambo vp?nimefurahi kusikia kijana mwenzangu umenufaika kupitia hivyo ni jambo la heri, swali langu naomba nipate address ya blog yako!
 
Vijana kwa wazee. Tujitahidi kuzitambua fursa za kujiajiri ili tuweze kujipatia manufaa yetu binafsi; manufaa ya jamii zetu na taifa kwa ujumla. Tambua kuwa, kila siku zinavyokwenda mafanikio ktk soko la ajira yanazidi kuwa finyu zaidi na zaidi. Tafakari, chukua maamuzi kisha thubutu. Siri ya mafanikio ni kwanza kumuweka Mwenyezimungu mbele, kujiamini na kisha kufanya kazi kwa bidii.
 
Big up kaka. Nadhani ulipokuwa shule hukuwa MCHOYO WA ELIMU.. ni wachache sana kama wewe. Endelea hivyo utafika mbali.

Asante sana. Wajua, elimu yote ni ya Mwenyezimungu. Ni amana yake aliyotutunuku wanadamu. Wengi hawajui kuwa unapogawa elimu, moja kwa moja unakuwa umefanya ibada. Na malipo yk ni makubwa. Na ni nani mlipaji Mkuu kama Yeye Maulana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…