Nimejiajiri kama Blogger, hata nawe unaweza jaribu

Nimejiajiri kama Blogger, hata nawe unaweza jaribu

Mkuu shukrani kwa darasa, nimejaribu kfungua nimeweza lakini kuna gharama natakiwa kuchangia. naomba unifahamishe nitachangia gharama hizo kwa muda gani?
 
Mjasiriamali M hongera kwa jitihada zako, kwa kifupi mianya katika blogs, website na youtube bado ni mikubwa sana katika tz kwa kuwa vitu vingi sana ambavyo viko online katika nchi nyingine bado havijawekwa online. Usiishie kwenye google free blog tu, endelea kufikiria kitu gani muhimu ambacho unaona watu wanahitaji lakini kinapatiana kwa taabu mfano wa zoom n.k pia unaweza kuanzisha youtube chaneel ila inabidi uwe mbunifu sana ku-appload video let say weekly na kupata viewz labda 10k kwa kuanzia google hugawa share of ad revenue may be usd 1-4 per 1000 view lakini wako makini sana kwenye originality uki-appload kazi yeyote ya mtu mwinginw lets say music, au hata beat au chochote big part of revenue itaenda kwa huyo mmiliki halali.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu shukrani kwa darasa, nimejaribu kfungua nimeweza lakini kuna gharama natakiwa kuchangia. naomba unifahamishe nitachangia gharama hizo kwa muda gani?
Gharama kwa Adsense au Google bloger kaka? Adsense kama utaomba kama publisher ni bure kazi ni kwa wao kukulipa wewe kutokana na spidi ya watu na matangazo katika site yako, au kama ni blogger blog ni bure labda kama utahitaji iwe na domain yako badala ya .blogspot ndo unalipia $10, sijui nimekujibu mkuu?
 
Mjasiriamali M hongera kwa jitihada zako, kwa kifupi mianya katika blogs, website na youtube bado ni mikubwa sana katika tz kwa kuwa vitu vingi sana ambavyo viko online katika nchi nyingine bado havijawekwa online. Usiishie kwenye google free blog tu, endelea kufikiria kitu gani muhimu ambacho unaona watu wanahitaji lakini kinapatiana kwa taabu mfano wa zoom n.k pia unaweza kuanzisha youtube chaneel ila inabidi uwe mbunifu sana ku-appload video let say weekly na kupata viewz labda 10k kwa kuanzia google hugawa share of ad revenue may be usd 1-4 per 1000 view lakini wako makini sana kwenye originality uki-appload kazi yeyote ya mtu mwinginw lets say music, au hata beat au chochote big part of revenue itaenda kwa huyo mmiliki halali.
Nimekupata Kaka, thanks for the heads up, hata mimi nna ndoto kubwa sana na huu uwanja wa "Online" hapa kwetu, Mola akituwezesha tutafika mbali kwani wapo wenye mawazo mazuri sana huku, lakini hawajapata wa kuwaamsha, Shukran kaka wehoodie .
 
Habari ndugu zangu, leo naomba nami niongee neno katika uwanja huu wa kijasiriamali, Mimi ni mhitimu wa Degree ya Uhasibu miaka 3 iliyopita, tangu kipindi hicho chote sijapata ajira ya kudumu na rasmi, Namshukuru Mungu niliwahi kusomea mambo ya I.T kwa level ya Certificate nilivyomaliza Form 6 mwaka 2007, sasa baasi, baada ya kusota miaka yote huku nikihangaika kwa hili na lile, nikapata wazo la kuwa Blogger, ingawa mwanzoni ilikuwa ngumu lakini sikuacha kujituma na kujifunza toka kwa waliofanikiwa kwani hata wao walianzia chini. Kwa muda wa miezi sita ya mwanzo nilikosa Direction nzuri kwani kila kitu nilikuwa nataka kufanya au kuandika mimi, kuna kipindi nilikata tamaa na kuona kwamba Kupata mafanikio kupitia Blogging si kwangu mimi, hata hivyo kipindi hicho kigumu kilipita na nikapata kibarua fulani ambacho kilinifanya nijitume na kujikusanya katika suala zima la fedha na kuweza kununua laptop mpya na universal modem ambavyo ndio kama JEMBE na SHOKA langu.

Baada ya hapo nilijipanga kwa kuwa naandika Articles zenye kuvuta hisia za wasomaji wangu huku nikiendelea kujifunza nami kadri siku zinavyoenda. Kwa uchache nawashauri Vijana wenzangu ambao tuna access na internet na tuna muda kujifunza na kufanya hivyo kwani mimi nimeanza kuyaonja matunda ya blogging kupitia Google Adsense kwani hata leo nimetoka kuchukua Hela zangu Kupitia Western Union. Pia binafsi nimeanzisha blog ambayo tutakuwa tunaelekezana na kufundishana mambo mbali mbali ikiwemo na mbinu za kufanya ili kufikia mbali katika blogging.

Kwa vile si mtaalamu sana wa ki teknolojia na computer science ntakuwa natoa facts ambazo hata mimi mhasibu nilizipitia na mpaka leo nami napata kidogo kupitia Google Adsense.
Tafadhali tembelea Tanzania Bloggers | Mabadiliko Chanya katika Blogs Tanzania tuna mengi ya kuelezana.

email:tzbloggers@gmail.com

HATA HII MKUU
http://StartReferralJob.com/index.php?refcode=126339
 
Hizo zina kuwa na utata kidogo maana nyingi huwamalizia watu muda na hela wasiwape angalia link hizi uone malalamiko:-
StartReferralJob.com Reviews | Scambook
StartReferralJob (startreferraljob.com)
[Review] Is StartReferralJob a Scam? Fake Or Legal? Take a Chance To Read - MabZiCLe

na nyingine kibao hao si wakweli, maana hakuna hela ya kupatikana kirahisi hivyo, sijui labda.....!!!
 
Napenda sana mambo haya ya making money online na nimekuwa nkifatilia sana ila huwa napata tabu ktk kutengeneza blog na mambo ya domain coz wananipa option za kununua.cjasoma IT ila nnayo idea kubwa ya mambo ya internetting.nataka tufanye kazi pamoja no.zangu ni 0659626782.ukiwa tayari njulishe nkutafute.
 
ya hata nami natamani ila bado sijajua nitapataje pesa kupitia blogs nigeini madini maana nina ka blog kangu ila sijui nifanyeje nipate hizo pesa
 
NYONGEZA YA USHAURI:-

Kwa kipindi Kirefu kiasi nimekuwa katika mambo haya ya Blogging, nimeona na kujifunza mengi, nitoe wito kwa Vijana wenzangu ambao bado hatujapata Ajira Rasmi au wale ambao tupo kwemye Ajira na Tunafikiria Wapi tunaweza kupata nafasi ya kuanzisha Biashara ama Kuwekeza, basi Angalia na Karibu katika Ulimwengu wa Blogging, Ni Zao la kipekee ambalo endapo utalilima na kulilea kwa Misingi inayotakiwa kamwe haliwezi kukutupa Ingawa Lina Changamoto Nyingi. Karibu Tujadiliane na Kupeana Njia zaidi. Kila la Kheri kwa wote watakao kuwa tayari kuthubutu.

Mabadiliko chanya, yanaanza sasa.
 
Back
Top Bottom