nimejifunza kitu hapa ingawa ni kichekeaho

nimejifunza kitu hapa ingawa ni kichekeaho

maukison

New Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
2
Reaction score
6
KWA WANAUME:

[emoji109]Wanaume walikuwa kwenye semina wakaulizwa. Mara ya mwisho kumwambia mkeo unampenda ni lini? Wengine wakasema leo asubuhi, wengine muda sio mrefu. Muwezeshaji akawaambia kila mmoja sasa hivi amuandikie mkewe sms amwambie nakupenda mke wangu halafu badilishaneni simu kila mmoja asome maajibu ya mwenzake. Majibu yalikuwa hv:
1. Unaota au?
2. Umekumbwa na nn?
3. ??!! Makubwa!
4. Utanieleza hii sms ulikuwa unamtumia nani.
5. Leo sikusamehi najua kuna kitu.
6. Huyo ulienae ndo kakwambia unitumie hii sms?
7. Najua tu tayari kuna kitu umeharibu.
8. Wewe sema unachotaka.
9. Leo hunipati ng'o!
10. Nani mwenzangu
 
Huo ndio ukweli kwa sisi waafrika wengi kumwambia mkeo/mmeo kwamba unampenda ni MSAMIATI mgumu Sana kuutamka labda kwenye bongo muvi tu?!
 
Hahaha hii nimeipenda[emoji1] [emoji1]
 
Yaani mke anakujibu "nani mwenzangu" ina maana hata namba ya mmewe hana
 
Hahahaha kweli funzo kwa wapendanao
 
Back
Top Bottom