mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 704
- 2,435
Kujikagua na kujipima ni jambo la muhimu sana , hebu tafakari miaka mitano yako nyuma na sasa, huko ulimiliki nini na sasa unamilki nini , shughuli zako za kiuchumi je zimetanuka na atleast zinatosheleza mahitaji yako au bado mechi Ngumu sana upande wako ukichukua muda wako ukajitenga na kukaa chini na kujiuliza kwa umakini sana nini umefanya kwa miaka iliyopita na unajiona wapi miaka mitano ijayo inatisha sana ule mtazamo uliokuwa nao wakati wa ujana kuhusu maisha bado unao ule ule, zarau ulizokuwa nazo enzi hizo kuhusu watu wazima unapowaona wanaishi maisha magumu bado unazo, unaipa elimu ya darasani asilimia ngapi kwenye mchango wa kipato chako , vipi ajira yako inatosheleza kipato chako ? vitu vingi ukijiuliza vinatia hasira sana
Mimi binafsi nimejitafakafari nimejikuta kwenye huzuni tu ,ndio napiga hatua , ndio yapo mabadiliko fulani lakini bado sana , zipo transactions ambazo nilikuwa siwezi kufanya sasa nafanya bado mechi ni ngumu sana upande wangu , kipato nilichonacho hakinipi nguvu ya kusimama mbele za watu kama mtu ninayejiamini, nauchukia sana umaskini lakini bado hautaki kunitoka , nahisi kuna umuhimu wa kubadili mbinu za utafutaji ila tu zisihusu uchawi, uporaji na utapeli , nahisi kuongeza muda wa kufanya kazi na kuongeza muda wa kuomba MUNGU