Nimejikusanya na kupata 350,000; TRA wananikadiria kodi kubwa, nifanyeje?

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
Nimejipigapiga na kupata sh.350,0000/= Laki tatu na nusu.

Niliwahi kuwaomba ushauri mkasema nifungue genge. Nashukuru nimefanya hivyo pamoja na kufungua kaduka kadogo kwani genge limenigharimu sh.100000/= tu na linakwenda vizuri.

Sasa kwa kuwa nimedhamiria biashara ya kuuza vitu vidogo vidogo vya nyumbani nilienda TRA ili wanipe TIN NUMBER kwa sababu nina mpango wa kuwa wakala wa Mpesa, tigopesa, Airtelmoney na Halopesa.

Wamenikadiria na kusema nipeleke sh.318,000/= Laki tatu elfu kumi na nane kama kodi kwa miezi 6.Wakaniuliza anza kulipia sasa nikasema sina pesa yoyote, yule mama akachukue ile tin namba yangu na kuihifadhi kasema nitakapoanza kulipia niende na fomu moja hivi aliyonipa.

Sasa wadau fomu imeandikwa expected annual income is tsh.8000000/=Hiyo ninini?Kingine,hiyo kodi mbona naona kama ni kubwa, incase nikishindwa nifanye nini?

Naombeni ushauri wadau. LENGO MIMI NI MUUMINI MZURI WA MAENDELEO NDIYO MAANA SITAKI KUKWEPA KULIPA KODI KWANI HATA NILIPOENDA TRA WANIKADIRIE JIRANI ZANGU WOTE AMBAO WANAFANYA SHUGHULI KAMA ZANGU NA HAWALIPI KODI WANANIONA ZUZU.
 
Hongera kwa kuwa mzalendo mkuu....ulienda kuchukua TIN kwa ajili ya GENGE au ajil ya kuwa wakala wa huduma za simu kwenye miamala(transction)...?.....ukishidwa kulipa funga biashara waandikie barua kuwa umefunga biashara uki ukitaja sababu ya kufunga.....Pia kuchekwa na watu usijali mkuu wewe piga kazi tu
 
Genge nimeweka mbele ya kaduka kangu.Nauza dagaa,piripiri,hoho,vitunguu,karoti,nyanya,limao na tangawizi.
 
Walikuuliza mauzo yako kwa siku? Kama walikuuliza uliwaambia ukweli?

Kama uliwaambia ukweli basi wanachukua mauzo yako wanazidisha mara mwaka mmoja alafu ndio wanakukadiria kodi.

Mimi kama mauzo yangu ni 100,000/= au 200,000/= huwa nawaambia kuwa mauzo yangu ni 20,000/=au 30,000/=.

Sasa kijana kama genge lako linauza sh 150,000/= au 200,000/= na ukawaambia ukweli [emoji16][emoji16]
Jua ndio maana ulilipishwa kodi kubwa namna hiyo.

Ushauri wangu kwako ni kwamba fanya kazi kwanza alafu siku ukishatajirika ndio uanze kulipa kodi.
Genge la matunda hapaswi kulipa kodi mkuu
 
Hivi hawa TRA ni raia wa wapi?

Hivi wanajua kweli maana halisi ya maneno MRADI WA GENGE?

Kweli kabisa biashara ya genge unamkadiria mtu 8m? Hili sio genge, ni supermarket labda.
 
Hivi hawa TRA ni raia wa wapi?

Hivi wanajua kweli maana halisi ya maneno MRADI WA GENGE?

Kweli kabisa biashara ya genge unamkadiria mtu 8m? Hili sio genge, ni supermarket labda.
Mkuu 8m ni annual sales turnover ya huyu mwenye genge. Ameangukia kwenye category hiyo kutokana na maelezo yake mwenyewe. Usikimbilie kuhukumu pasipo ufahamu au kujiridhisha.
Ukitaka kufahamu kivipi TRA wanakadilia kodi, tembelea ofisi zao zilizo karibu na eneo lako.
 
Swadaqta Mkuu. Nimekusoma.
 
Hivi hawa TRA ni raia wa wapi?

Hivi wanajua kweli maana halisi ya maneno MRADI WA GENGE?

Kweli kabisa biashara ya genge unamkadiria mtu 8m? Hili sio genge, ni supermarket labda.
Tra wanaangalia mauzo mkuu. Hawaangalii mtaji
 
System ya TRA na Usimamizi wa biashara nchini kwa ujumla sio rafiki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati. Kwa wafanyabiashara wakubwa ndo maana wanakuwa vinara wa kukwepa kodi!
 
Mtoa mada umeangalia vizuri tarakimu na maneno kuwa yanaoana vema kwenye fomu zako lakini? Maana hata hapo juu umesema laki tatu na nusu lakini hizo namba zinasoma milioni tatu na nusu!
 
Ndugu,MIPANGO nakiri nimekosea kuandika.Kimsingi mtaji wangu ni sh.350,000/=laki tatu na nusu.

Nakwambia siku waliponikadiria kodi mimi mbele yangu alikuwepo babu mmoja alilia baada ya kutajiwa kodi yake.

Nikamsikia akilalamika kwa dada aliyetukadiria kuwa inakuwaje kodi na mtaji vinalingana yule dada wa TRA wala hakumjali akamwambia nifanyeje sasa kwa sababu mimi naingiza kwenye system hizo data zako system ndiyo inaleta kiasi cha kodi!!!
 
Tatizo la biashara ndogo wanalipa presumptive tax ndo mana mambo yanakuwa hivi, hao maafisa kodi wala hawajisumbuagi maana wanajua wengi wafanyabiashara wadogo hawana knowledge na masuala ya kodi, kwa hiyo wanajipigia tu bila kuangalia uhalisia.
 
Wewe unataka kuchosha watu tu hapa.. Expected Annual Income ya 9 Million kodi yake ni 318,000 kwa Mwaka si kwa miezi sita kama unavyodai..
 
Tatizo la biashara ndogo wanalipa presumptive tax ndo mana mambo yanakuwa hivi, hao maafisa kodi wala hawajisumbuagi maana wanajua wengi wafanyabiashara wadogo hawana knowledge na masuala ya kodi, kwa hiyo wanajipigia tu bila kuangalia uhalisia.

Si kweli kwamba wanajipigia tu wanavyotaka.. Kuna guide book yao ambayo wanaifata kwa aina za biashara ambazo hazina vitabu vya mahesabu
 
Lipa kodi kijana, ila hata mimi ningekucheka ungekuwa karibu.
Usiwe lofa ww estimated annual income ya huyo ni too much na ukizingatia hana kampun kubafff sas umcheke kwa lipi wakat kosa ni la TRA.? kuna kampun ya Bima hapa dsm inalipa 134,500 annually na ina branch kama 4 hvi zikiwemo Posta, Msasan na Sinza huko sas kwa muuza Genge analipishwa 318,000 unajisif kabisa eti ungemcheka hvi ni akil au utaahira.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…