Nimejipanga kuroga

Nimejipanga kuroga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Leo nakamata ungo,tuone mtarukaje
So kwamba ninamsongo,hii ni toroka uje
Umetimia mpango,pona yenu bora mje
Nimejipanga kuloga,muiteni baba yenu.


Mlinirusha kilinge,enzi za mababu wenu
Nasema na mjipange,,chelewa shauri yenu
Mlininyanganya tonge,kisa ni nyumbani kwenu
Nimejipanga kuloga,muiteni baba yenu.

Hakyanani mtalipa,mkitaka msitake
Panya nimekua papa,nasubiri mropoke
Vidonge leo nawapa.tasema hadi nichoke
Nimejipanga kuloga,muiteni baba yenu.

Hata kama ni zamani,bado nina kukumbuka
Tukutane kijiweni,tujue wakuumbuka
Nasema nawalogeni,na leo patachimbika
Nimejipanga kuloga,muiteni baba yenu.

iddyallyninga@gmail.com
 
Hakyanani nimejipanga kuloga kizazi cha kwanza hadi cha nne cha walionitenda uovu!
 
Back
Top Bottom