HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,567
Dear Wana MMU,
Shukrani za kipekee ziwafike kwa michango yenu ambayo binafsi, naamini imemnufaisha kila mmoja wetu si tu kwa mada ziliopostiwa hata kwa comments za wadau zenye ushauri mzuri wa kufariji, kuelimisha sometimes na jokes za hapa na pale za kukufanya uipende JF!
Kuna wengine wamenufaika kwa kupata marafiki, wachumba, kazi, deal za pesa, kuondoa upweke, msongo wa mawazo nk, lakini pia wapo waliokuwa addicted sana na JF kiasi hata cha kushindwa kumaliza kazi zao muhimu za kiofisi kwa wakati, na kuzorotesha performance za makampuni yao! Kuna wengine wamekuwa wakichelewa hata kulala kwa ajili ya JF!
Wapo waliotoa ushauri mbaya kwa kukusudia au kutokukusudia na kujikuta wamevunja mahusiano ya watu. Binafsi sikufurahia, ila tunawaombea maana kwa uhalisia kila mtu ana mtazamo wake na kila alifanyalo mtu ni sahihi sana mbele ya macho yake mwenyewe hata kama ni baya!
Tunapoelekea kwenye Christmas na mwaka mpya, wana JF tumuombe Mungu atusamehe kwa yote mabaya tuliyoyafanya kwa mwaka huu na kuyaacha. Tujitahidi kuwa watu wema, waungwana, tusio na hila wala lawama mioyoni mwetu.
Tushauri ktk kujenga na kuimarisha ndoa na mahusiano ya watu huku tukijitahidi kuondoa infidelity na fikra za maovu.Comments zetu zisitazame hoja imepostiwa na nani bali msg iliyomo bila kuipinga hoja ya mtu kwa kuendekeza chuki binafsi.
Tujichunge na UKIMWI, tujitume makazini, tuache ubinafsi, tupige vita rushwa, tuchukie na kupiga vita ufisadi, tuwe wazalendo kwa nchi yetu, tuchague viongozi wachapa kazi wenye sifa, tuache dharau, na tuweke mipango ya maendeleo ili tuweze kuwa na maisha bora na kuijenga nchi yetu.
Na kwa wale Kupe waliozoea kusoma humu topics za wengine na kucopy na kuwatumia wengine kwenye emails kana kwamba wameziandika wao bila kutoa mchango wowote hapa jukwaani, mjirekebishe, msilitumie jukwaa hili kwa manufaa yenu binafsi, huo ni unyonyaji!
Nawataki kila lililo jema na mafanikio mema ktk mwaka ujao. Mfanikiwe makzini,kwenye biashara na shughuli binafsi. Mungu akutane na mahitaji ya mioyo yenu. Baraka zake, upendo na ulinzi wake uwe nanyi daima.
Kila la kheri,
HorsePower :A S 465: