Ni misimamo yangu kwamba;
- Sipandi bodaboda isiyo kuwa na kioo (side mirror), maana mambo ya kugeuziwa shingo kila muda ujinga huo sitaki, Mara ageuke nyuma akosee tuelekee mtaroni spendi kabisa!
- Sipandi bodaboda ya bonge au mtu mwenye kitambi; Haiwezekani mi nilipe buku halafu siti yote akalie yeye bure mimi nikae kwenye chuma (value for money)
- Sipandi bodaboda ya mtu mfupi Mimi, ujasiri huo sina, Mambo ya kuwekana roho juujuu kwenye mchanga au utelezi siyataki, maana miguu yake haifiki chini hadi nimsaidie mimi kukanyaga chini.
- Sipandi boda boda yenye na dreva aliyevaa singirendi yenye kuonyesha makwapa!
- Sipandi bodaboda anaesalimia kila mtu njiani mimi siyo mgombea sina ukarimu huo
- Sipandi bodaboda ya yule kiduku anaekalia tako upande upande mawenge sitaki!
- Mwisho ingawa siyo kwa umuhimu, Bodaboda mwenye kujidai ana haraka kuliko mimi abiria huwa naomba anishushe ili nimuache awahi anakoenda!