Nimekaa kwenye mahusiano miezi 7 na mtu ambaye sikudhania

Nimekaa kwenye mahusiano miezi 7 na mtu ambaye sikudhania

Gepard

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2021
Posts
291
Reaction score
385
Mwaka 2018 nlienda kumsalimia dogo wangu wa kiume shuleni kwao boarding. Kipindi hicho nipo chuo mwaka wa pili. Tulipiga story sanaa na kuzunguka mazingira ya shule, akanitambulisha kwa marafiki zake wengi wakiume na wakike pia. Kwa kweli ni mtu wa watu. Kwa hili: , Dogo popote ulipo kaka yako Gepard nakukubali🤝.

Nakumbuka alinitambulisha kwa marafiki zake wa kike zaidi ya 50, kina Eliza, Neema, Winny(huyu ndio nlichanganya jina lake nikamkumbuka Kama Queen), Veronica nk. Ila kwa kweli Winny nlivutiwa nae, sikutaka kuonesha kama nlimpenda kwa mda ule ila moyoni nlisema ntatafuta mawasiliano naye.

Kumbe jina nlichanganya hakuwa Queen alikuwa ni Winny ila pia alikuwepo mwanafunzi alieitwa Queen. Baada ya miezi kupita nkamuomba dogo namba ya Queen ila kiuhalisia ni Winny ndio nlikuwa namaanisha. Baada ya kupata namba nliwasiliana nae na kumpiga sound akanielewa mana alinifahamu kupitia dogo.

Nakumbuka hakuwa na smartphone wala social media hakuwepo. Stress za mapenzi tulishare, shida na raha. Kunitambulisha kwa wadogo zake na marafiki zake. Siku tunakutana baada ya yeye kumaliza form 6 kumbe sio niliekuwa namdhania ila mwingine kabisa ambae sikutegemea na alikuwa mzuri zaidi ya nliokuwa namfikiria. baada ya kumuona tu nlipigwa na butwaa Kwanzaa, nkamuambia ndio wewe akanambia hunijui kwani?

Nikasema nmeshakukumbuka ila umebadilika dear moyoni nkijua kabisa sio yeye. Nlijiadjust tu story nyingi huku furaha ya kupindukia nlikuwa nayo. tulikaa kwenye relationship baada ya kuzoeana nlimueleza kisa chote akabak anatabasamu tu na kusema ni Kama alijua.

Pia, alikiri kuwa hata yeye alipata waswas nyuma kwa kuwa aligundua kama nlimchanganya kutokana na mazungunzo yangu. Kuna siku aliniambia hv Mimi nipoje nakumbuka nlitoa maelezo ya Winny asilimia zaid ya 50 sema Kuna vitu tu walishare But haikuwa suala kwake maana alinipenda pia Wala hakutaka kunipoteza.
 
Enhee ikawaje
Nlipigwa na butwaa Kwanzaa, nkamuambia ndio wewe akanambia hunijui kwani? Nkasema nmeshakukumbuka ila umebadilika dear moyoni nkijua kabisa sio yeye. Nlijiadjust tu story nyingi huku furaha ya kupindukia nlikuwa nayo. Ila tulikaa nae baada ya kuzoeana nlimueleza kisa chote akabak anatabasamu tu. Ila alikiri kuwa hata yeye alipata waswas nyuma kwa kuwa aligundua kama nlimchanganya. But haikuwa suala kwake maana alinipenda pia
 
Back
Top Bottom