BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Asante Kamanda! Unaweza kuwa baba upande wa mume harusi in 10 years, tuombeane heri. Ushanifahamu?
Ahsante sana Mkuu kwa kunipa heshima kubwa sana, lakini naona imenizidi kimo lakini kwenye majaliwa tutakuwa wote katika jambo hili la heri. Kwa maoni yangu kama huyu binti mnapendana kiasi hicho basi miaka 10 ya uBF na uGF ni mingi mno. Binti anaweza kukata tamaa mapema na kuingia mitini hasa ukitilia maanani biological clock ya wenzetu haina muda mrefu sana. Hebu lifikirie tena hili ili kupunguza kiwango hicho cha miaka 10 na labda kubakisha one third ya miaka hiyo. Kila la heri.