nakumbuka mara ya kwanza kufikiria kujenga nyumba, nilijenga ilipofika kwenye lenta, nikawa na hela nyingine mfukoni ghafla nikaona kuna kiwanja kizuriiii sehemu nyingine na cha bei ya chini, nikatumia ile hela kwenda kununua kiwanja hicho, nikaanza kujenga na chenyewe kufika kwenye lenta, nikaona bonge la uwanja sehemu nzuri jamaa anauza ana matatizo na ni hot keki na ni sehemu nzuri na uzunguni zaidi kuishi kuliko zile za awali, nikasimama unjenzi nikaenda kununua kiwanja hicho, kama zari la mentali kila nikifika, nikapata kiwanja kingine tena cha barabarani kwa ajili ya maduka. ilifika kipindi nikajikuta nina mapagale matatu na kiwanja mkononi na bado napanga.