Rene Jr.
JF-Expert Member
- Jan 31, 2014
- 3,714
- 2,376
Salaam wakuu,
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka, mwenzenu nimekwama hivyo naangalia upande wa pili. Nilikuwa na kazi zangu za kijasiriamali kwa miaka kadhaa, mambo si mambo yakatukia ya kutukia nikaanguka, I just dont have the luxury to give up, najaribu kuinuka na kujikung'uta vumbi niangalie usawa mwingine wa kusonga mbele.
Nimejaribu kuangalia options kibao, lakini kila iliyopo kichwani inahitaji pesa ambazo sina!! Baada ya kuwaza ndugu jamaa na marafiki nikawaza JF, najua kuna watu wengi humu wanaweza kunisaidia na mimi nikawasaidia nguvu na akili katika kazi zao. Mimi niko flexible sana wakuu nafanya kazi yoyote popote, Kama una shamba sehemu unahitaji mtu wa kusimamia mi ntavaa buti na kuhamia huko, kama una ofisi sehem unahitaji mtu mwenye knowledge ya IT nitavaa tai na nitashinda na kukesha nyuma ya computer, lengo nikufurahishe katika kazi yako uone tofauti katika utendaji na uzalishaji ili mwisho wa mwezi na mimi unifurahishe nijikusanyie kijimtaji cha kulianzisha tena, maana mwenzenu nina familia ya mke na watoto wawili, posho ya mama haitoshi kitu.
Mara zote huwa najitahidi kuangalia mambo upande chanya, nina imani hapa kuna watu wanaoweza kunisaidia, KAZI YOYOTE WAKUU MI NAFANYA, alimradi tuelewane maslahi na majukumu tu.
Nakaribisha majadiliano PM, pia kama kuna mambo unapenda kufahamu.
Natanguliza shukrani.