Health service
Member
- Mar 8, 2014
- 60
- 11
- Thread starter
-
- #21
Vaa tu miwani hakuna jinsi matatizo mengine ya macho ni ya kurithi,mimi nina tatizo la kutokuona mbali miaka kumi sasa navaa miwani, madaktari hawashauri kufanyiwa operation na ujana utaharibu macho,operation ni kwa wazee wasioona sana.
Pole ndg macho yanauma?
hivi uumwe macho kiukwelikweli na unaambiwa uvae miwani utakataaje? mbona watu wanavaa miwani na maisha yanasonga mbele!?na ujue cku zinavyozidi kusonga ndo yanazidi kuharibika!
Pia inategemea na umri wako................................. ni miakamingapi?Habari wa jukwaa letu la lfdoctor?
Jamani nimekata tamaa ya kupona macho, nimetembea kwenye hospital nyingi tu naambiwa hawaoni tatizo wananipa tu ushauri wa kula vyakula na matunda na pia kutumia miwani ili kurekebisha uono hafifu, hii ina maana kuwa hospital hakuna tiba ya macho zaidi ya kupewa miwani tu.
Mimi binafsi sipendi kutumia miwani bali ni kupona kabisa tatizo la macho, niliwahi kuambiwa nimechezewa lakini hata tiba za jadi hazijanisaidia zaidi ya kufuja pesa. naombeni ushauri wadau nifanyeje?
Mkuu njoo nikupeleke kwenye maombi uombewe,kama una amimi na una nia nijulishe nikuagize sehemu ya maombi hakika utapona,lisilowezekana kwa binadamu,kwa Mungu lawezekana
Pia inategemea na umri wako................................. ni miakamingapi?
km umeweza kupost bila miwani basi Hongera
lkn km una zaidi ya 45yrs basi MIWANI ni lazima
Fika kwenye vituo vya Macho upimwe km tatizo ni kuona mbali au karibu utapatiwa miwani itakayorekebisha
Mkuu acha imani potofu wakuchezee macho ili iweje wakati umejiexpose kwenye region ambayo kuumwa macho ni kawaida sana(Dodoma)! Ulizani wale wagogo ombaomba huku mijini wamejitia minyaa eee!? Fuata ushauri wa daktari mkuu kugomea miwani unajikomoa mwenyewe!
wewe utakuwa mgonjwa mbishi,ungefuata ushauri wa ccbrt kama walivyokwambia coz they r da best,unaleta usharobaro hutaki kuvaa miwani wakati ungevaa mfululizo ungepona na kuacha kuivaa kabisa
Wapi nimesema situmii miwani au siitaki? mimi natumia miwani ila natafuta tiba.
sasa tiba yenyewe si ndio hiyo miwani kaka yangu,kubaliana na hali halisi,muhimu ni kupona na si kuchukia matibabu
Nenda kwa Dr. Ndodi kama sijakosea jina.......
Anapatikana wapi? na je naweza kupata mawasiliano yake?
Anapatikana Dar....kusema kweli contact sina. But nilikua na ndugu yangu alikua na matatizo ya macho.....Muhimbili wakasema afanyiwe operations kila mwezi for the rest of her life🙁
Tukaghairi....baada ya kupata ushauri kwa watu ndo tukaenda kwa huyo docta wa mimea ya asili..... aliponea hapo.
Just tafuta watu uwaulize kuhusu huyo Dr. Ndodi sijui Ngugi.... jina linanitatiza
Nashukuru! ila mkuu ndugu yako alitibiwa kwa muda gani hadi kupona? na je tatizo ni la lini?
Alipewa dawa akawa anachemsha sijui sasa alikua anakunywa tu au anadondoshea na matone.
Ila alisumbuliwa kama 3years hivi......tukahangaika sana
Alikuwa anasumbuliwa kwa namna ya kutoona mbali au macho kuuma? je unaweza kuniambia alitibiwa mwaka gani na kwa bei gani ili nikadilie kabla ya kumtafuta?
Matatizo hayafanani. Mtafute doctor akusikilize then yeye ndio atajua tiba.
Kama 2years back ndo alitibiwa. Mtafute hata google....Dr. Ndodi