Nimekataa kuwa miongoni mwa wasiojua kuongea Kiingereza kwa unyoofu

Ufafanuzi kidogo Dr. Haya Land, kama hutojali🙏

"Focus katika eneo lakini ambalo utaweza kulifanyika kazi"

Unaweza ukanifafanulia zaidi?


Hapa nimemaniisha kuwa lugha ya kiingereza ni pana Sana , hivyo hauwezi ukajua kila kitu Ila unaweza kuwa fluency kwa kuwekeza katika eneo lako la kazi.


Kupitia eneo lako la kazi unabidi kuwa unalimudu vizuri kupitia kiingereza

Mfano labda wewe ni Psychologist basi uwe na uwezo wa kujua kuwasiliana na kuwasilisha kwa lugha ya kiingereza .

Ukitumia mbinu hii utakuwa na competence katika kazi yako then utakuwa Fluency kwa haraka.

Ila ukitaka kujua kila kitu utakosa Hyper focus /mastering utajikuta unajua kiingereza Ila hauna uwezo wa kuitumia katika kazi yako hapo ndo utaonekana haujui na hii ndo inawakuta graduate wengi.
 
Ukijua English unaweza kwenda popote duniani na ukawasiliana na watu wa huko.English ndio lugha,Lugha kama kiswahili haikufikishi popote
 
Huu unyonge wa kutokuongea kiingereza vema niliukataa tangu nikiwa shule ya msingi. Sina elimu kubwa sana ya kusisimua siku moja nilijikuta nimehudhuria mkutano wa taasisi ya Mkapa Fellow pale mlimani city jijini dar, Lugha kuu ilikuwa ni kiingereza, nilitakiwa niulize swali na nichangie mada kwa kiingereza na elimu yangu ni ndogo ukilinganisha na washiriki wengine waliokuwa na elimu kubwa kuliko yangu. Nilijiamini nitaweza kuongea kwa ufasaha huku kamera za media mbalimbali zikinimulika na mbele yangu high table yupo mheshimiwa Mkapa, nilikatafuna kama maji kiingereza wanaigeria na wahindi wakasome. Kwa sasa najifunza kifaransa niko hatua za mwishomwisho, kiingereza nimeshatoka huko, ukija na british au american english tunapandisha tu bila kubabaika, leta hata kiingereza cha ireland sipati shida kuongea.
 
Tatizo watanzania wengi mara tu wanapohitimu elimu ya msingi au sekondari basi kiingereza huacha kuendelea kujifunza kwa bidii nje ya mfumo rasmi wa elimu. Elimu haina mwisho, mtu anatakiwa kuendelea kupata maarifa na stadi hata nje ya mfumo rasmi wa elimu, kusoma si lazima uwe shuleni/chuoni, popote panapoweza kujifunza jambo hukohuko unajifunza ili uweze kurahisisha mambo kwa wepesi na haraka zaidi. Dhana ya elimu ni pana haishii shuleni na chuoni tu, elimu ni bahari
 
Shukran sana mkuu
 
Akileta ngeli nampa kiswa kama nitatumia ngeli akisema mbovu aongee yangu sahihi
 
Ukijua English unaweza kwenda popote duniani na ukawasiliana na watu wa huko.English ndio lugha,Lugha kama kiswahili haikufikishi popote
Ni kweli kabisa mkuu.

Ndiyo maana Wakenya na Waganda waliopo ughaibuni ni wengi kuliko Watanzania.
 
Hongera sana mkuu
 
Ni kweli kabisa mkuu.

Ndiyo maana Wakenya na Waganda waliopo ughaibuni ni wengi kuliko Watanzania.
Yup kingereza ni lugha ya kimaraifa kila nchi unayoenda lazima utakuta wapo watu wanoielewa English,hata katika nchi ambazo wanaongea lugha zao kama China,Italy,Germany na nyinginezo.

Nashangaa wenye akili fupi wanaita utumwa kukitanguliza kiingereza mbele wanakionea ufahari kiswahili,jiulize kiswahili kinatupeleka wapi?.English ni Lugha ya vitu vingi science,technology na vingine vingi.Ukitaka upate maarifa mengi hasa kwenye Mtandao yanapatikana kwenye Lugha hii.I wish ningekijua kingereza sawia halafu kiswahili ndio kifuate.Nitaitwa mtumwa wa fikra ila wacha niseme ukweli huku nikitetemeka.
 
miaka ya elfu mbili na kumi nilikutana na dada wa kizungu pale Nando's.

nikaanza kumtongoza kwa kingereza cha ugoko maneno mpaka nitafute!.
ila wazungu waelewa aliwai kutambua kuwa kingereza sikijui akawa yeye ananisaidia maneno minikabaki"yah,,ok,,of corse.
 
Hiyo haina tofauti na mwajiriwa anayeamini bosi wake ni mjinga wakati bosi wake kaweza kubuni mradi na kumpa kazi inayompa mshahara kila mwezi.

Kama kuongea English ni utumwa na Kiswahili ni uzalendo, huo uzalendo umemfikisha wapi huyo "mzalendo" na utumwa wa English umemkosesha nini mwenye kukijua?

Utaona wazi kuwa Mswahili asiyejua lugha zingine ndiye anayekuwa kama mtumwa.

Nyerere asingejua English asingeweza kwenda UN kudai uhuru wa Tanganyika.
 
Hongera na Kila la kheri na Mafanikio katika azma yako. Wengi wa WaTz tumeanza kujifunza tangu chekechea, wengine darasa la 3, hivyo ni miaka mingi ya kujifunza, ila haikuwekewa mkazo sana, matokeo yake wengi katika utu uzima, bado inawapiga chenga.
 
Ukipata mtu anayependa kuzungumza kwa kiingereza na mkawa mnazungumza daily itasaidia saana.
Jiunge na app moja inaitwa hello talk unaweza kupata mtu wa kuexchange lang ukamfundisha kiswahili yeye akakufundisha kiingereza.
Au app ya Tandem pia jaribu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…