Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Huyu mpwa wangu nilimchukua kijijini miaka miwili iliyopita ili kuja kusoma haya masomo maarufu kama QT kwa maandalizi ya kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu. Ingawa alifaulu kwenda sekondari ya serikali wakati huo, lakini aliishia kidato cha pili baada ya kumimbishwa na mkware mmoja. Ilimlazimu kukaa nyumbani kwa takriban miaka mitatu akiwa hajui majaaliwa yake. Miaka miwili iliyopita nilipokwenda kijijini likizo niliona ni vyema nije naye huku mjini ili nimuendeleze kielimu.
Mwezi uliopita nilianza kusikia minongono kuwa kapata mchumba. Mimi kama kawaida yangu sikutaka kuingia kwenye udadisi kwa sababu haya mambo huwa yanaanzia kwa akina mama. Mwanzaoni mwa mwezi huu mama Ngina akanidokeza jambo hilo, lakini hakuwa amelipa uzito sana kwa sababu alikuwa anataka binti asome amalize ili apate na yeye mahali pa kusimamia. Lakini alinidokeza kuwa presha inatoka kwa shangazi zake yaani dada zangu.
Nilimuomba asubiri nizungumze na dada zangu ili kujua kinachoendelea. Lakini kabla ya kufanya hivyo, nikapata taarifa ya kuletwa posa, ilinishangaza kidogo. Ngoja nifupishe stori. Kwa kifupi ni kwamba niliwajulisha shangazi zake na wajomba zake walioko hapa mjini, kwani mama wa binti yuko kijijini na baba wa binti ni mtu wa kusafirisafiri lakini makazi yake ni kule mkoani Tanga. Nilizungumza na baba wa binti akaniambia amenikabidhi majukumu yote.
Siku ya kikao ilifika na walikuja wajomba wa binti mashangazi na ndugu wengine wa karibu. Posa ilifunguliwa na ndani ya bahasha kulikuwa na kama 20,000 na barua yenyewe ya posa. Nilimkabidhi mdogo wangu aisome na baada ya kuisoma, nikamuita binti na kumuuliza kama anafahamu lolote juu ya ile posa. Binti alikiri kuwa anaifahamu. Tukaanza usaili ili kujiridhisha na hapo ndipo kukazuka jambo ambalo karibu wanaume wote lilitutia shaka isipokuwa shangazi zake na binti walionekana kutojali.
Jambo lenyewe pale binti alipokiri kuwa mposaji anaishi na mwanamke mwingine na wameshazaa watoto wawili wakwanza miaka 4 na mwingine miaka 2 lakini hawana ndoa, hivyo huyo bwana ambaye ndio kwanza ametimiza miaka 35 anataka kumuacha huyo mwanamke amuoe mpwa wangu. Hilo mimi lilinitisha sana na nilitoa maelekezo ile posa irejeshwe kwa mwenyewe pamoja na 20,000 zake. Shangazi zake na binti walionekana kupingana na mimi, lakini nilitumia muda mwingi kuwaeleza madhara yanayoweza kumpata mpwa wangu iwapo atadandia ndoa za namna ile.
Kikao kiliisha na maamuzi yalifanyika lakini baadhi yao hawakuridhishwa na maamuzi yangu. Hivyo nimesikia kuna njama za kunizunguka posa ipelekwe Tanga kwa babaye lakini baada ya kuzungmza na baba na mama wa binti wamekubaliana na mimi kuwa ni niko sahihi. Hata hivyo baadae nimekuja kupata taarifa kuwa mposaji katembeza mkwanja kwa shangazi zake na binti ili waweke shinikizo posa ipokelewe, kwani walishanusa udaku kuwa sitakubaliana na posa hiyo kwa kuwa binti bado anasoma.