Nimekataa posa ya Myao kwa mpwa wangu…………………!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Huyu mpwa wangu nilimchukua kijijini miaka miwili iliyopita ili kuja kusoma haya masomo maarufu kama QT kwa maandalizi ya kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu. Ingawa alifaulu kwenda sekondari ya serikali wakati huo, lakini aliishia kidato cha pili baada ya kumimbishwa na mkware mmoja. Ilimlazimu kukaa nyumbani kwa takriban miaka mitatu akiwa hajui majaaliwa yake. Miaka miwili iliyopita nilipokwenda kijijini likizo niliona ni vyema nije naye huku mjini ili nimuendeleze kielimu.

Mwezi uliopita nilianza kusikia minong’ono kuwa kapata mchumba. Mimi kama kawaida yangu sikutaka kuingia kwenye udadisi kwa sababu haya mambo huwa yanaanzia kwa akina mama. Mwanzaoni mwa mwezi huu mama Ngina akanidokeza jambo hilo, lakini hakuwa amelipa uzito sana kwa sababu alikuwa anataka binti asome amalize ili apate na yeye mahali pa kusimamia. Lakini alinidokeza kuwa presha inatoka kwa shangazi zake yaani dada zangu.

Nilimuomba asubiri nizungumze na dada zangu ili kujua kinachoendelea. Lakini kabla ya kufanya hivyo, nikapata taarifa ya kuletwa posa, ilinishangaza kidogo. Ngoja nifupishe stori. Kwa kifupi ni kwamba niliwajulisha shangazi zake na wajomba zake walioko hapa mjini, kwani mama wa binti yuko kijijini na baba wa binti ni mtu wa kusafirisafiri lakini makazi yake ni kule mkoani Tanga. Nilizungumza na baba wa binti akaniambia amenikabidhi majukumu yote.

Siku ya kikao ilifika na walikuja wajomba wa binti mashangazi na ndugu wengine wa karibu. Posa ilifunguliwa na ndani ya bahasha kulikuwa na kama 20,000 na barua yenyewe ya posa. Nilimkabidhi mdogo wangu aisome na baada ya kuisoma, nikamuita binti na kumuuliza kama anafahamu lolote juu ya ile posa. Binti alikiri kuwa anaifahamu. Tukaanza usaili ili kujiridhisha na hapo ndipo kukazuka jambo ambalo karibu wanaume wote lilitutia shaka isipokuwa shangazi zake na binti walionekana kutojali.

Jambo lenyewe pale binti alipokiri kuwa mposaji anaishi na mwanamke mwingine na wameshazaa watoto wawili wakwanza miaka 4 na mwingine miaka 2 lakini hawana ndoa, hivyo huyo bwana ambaye ndio kwanza ametimiza miaka 35 anataka kumuacha huyo mwanamke amuoe mpwa wangu. Hilo mimi lilinitisha sana na nilitoa maelekezo ile posa irejeshwe kwa mwenyewe pamoja na 20,000 zake. Shangazi zake na binti walionekana kupingana na mimi, lakini nilitumia muda mwingi kuwaeleza madhara yanayoweza kumpata mpwa wangu iwapo atadandia ndoa za namna ile.

Kikao kiliisha na maamuzi yalifanyika lakini baadhi yao hawakuridhishwa na maamuzi yangu. Hivyo nimesikia kuna njama za kunizunguka posa ipelekwe Tanga kwa babaye lakini baada ya kuzungmza na baba na mama wa binti wamekubaliana na mimi kuwa ni niko sahihi. Hata hivyo baadae nimekuja kupata taarifa kuwa mposaji katembeza mkwanja kwa shangazi zake na binti ili waweke shinikizo posa ipokelewe, kwani walishanusa udaku kuwa sitakubaliana na posa hiyo kwa kuwa binti bado anasoma.
 
utamwoa wewe!!!!! hujui kuolewa ni bahati
Sitamuoa mimi, ataolewa na mwanaume mwingine lakini siyo Mhyao..................................LOL
Kwani uliambiwa mpwa wangu hana bahati?
 
wise decision coz km ndio kwanza ameanza kusoma then anawaza kuposwa tena na mlez upo purposely kuona binti anasoma, isingekua vyema kwako kumruhusu na kupokea posa hiyo; Angalizo ni kwamba km huyo binti kaja kusoma then still anawaza kuolewa wakati mambo bado mabichi kabisa kishule nawasiwasi sana na commitment yake huyo binti na shule na inawezekana kuwa wewe ndio unajali zaidi maisha yake but mwenyewe akawa hana mpango na shule so kwa picha hiyo km shangaz zake wapo kambi moja na binti wanaweza kumpampu atishie kuacha shule km wewe hutaki aolewe theni finali utakua umepoteza efforts zako bure kumbeba mtu asie bebeka :embarassed2:
 
utamwoa wewe!!!!! hujui kuolewa ni bahati

Mwanzoni niliwaza kumuuliza Mtambuzi hivyo hivyo lkn baada ya kusoma bandiko zima nimemuunga mkono Mtambuzi mia kwa mia.
Wewe akili zako ni kama shangazi za huyo binti; nachelea kusema Wanawake wote mna akili zinazofanana kwa kuwa wa kwangu hawezi kamwe kukubali upuuzi huo.
 

Nakushukuru mkuu, unajua nilimkuta kijijini na ana mtoto wa miaka miwili asiyejua hata seti tano ya baba yake..............Lengo langu ni kumsaidia aweze kusimama peke yake na amudu kumlea mwanae, lakini kaja mjini kadanganywa kidogo basi na yeye bila kujiuliza anakurupuka. hawa mabinti wakija mjini na kupaka Carolight na kupendeza basi inakuwa tabu, wanaume wakware nao hawachezi mbali.................................
 
Lakini Mtambuzi kwa story hii sidhani kama kuna msomaji hapo!
Unazunghumzia stori gani hapo...............Hili jambo kuna baadhi ya wadau humu pia niliwa-PM kuwataka ushauri. Kabla ya kuliweka humu kuna baadhi ya wana JF wanalifahamu...........................Hivi kumbe humu nishaonekana mtu wa tiralila..........eh!
 
Siungi mkono kuolewa kwake lakini mna uhakika kuwa atasoma kweli?Atakuwa na interest na elimu?
Manake hawa mabinti wakishawaza kuolewa tu akili zao zinakuwa kama zimefungiwa injini za rocket,wanawaza kupaa tu.
 
Baba huyu complicater najuuuta mie..

Mimi niko makini, hata hawa wnangu kina Ngina unafikiri wataolewa tu na mijianaume isiyo na malengo.............Lazima niwa -Interview kwanza na kama hawana TEMBO CARD..........Posa haipokelewi
 
loh mtambuzi uko sahihi kabisa ila vibinty sijui vikoje viking"ang"ania jambo ni ishu yan utaona tuu siku kajipeleka mwenyewe.
komaa mwaya asome kwanza achane na ilo bazaz jaman...... ataolewa na wengineo loh.
 
Hata hivyo baadae nimekuja kupata taarifa kuwa mposaji katembeza mkwanja kwa shangazi zake na binti ili waweke shinikizo posa ipokelewe, kwani walishanusa udaku kuwa sitakubaliana na posa hiyo kwa kuwa binti bado anasoma.
Dunia aaa dunia yani mpaa kwenye posa kuna rushwa.
 
loh mtambuzi uko sahihi kabisa ila vibinty sijui vikoje viking"ang"ania jambo ni ishu yan utaona tuu siku kajipeleka mwenyewe. komaa mwaya asome kwanza achane na ilo bazaz jaman...... ataolewa na wengineo loh.
Mama Ngina alinidokeza kuwa kuna siku alimsikia akizungumza na huyo Mhyao wake kwa simu akiwa nyuma ya nyumba na inaonekana walikuwa wanapanga mikakati fulani..............kitu alichosikia ni kama vile anataka kufunguliwa biashara ya Saloon ya kike sijui ili kumuwezesha...............nasubiri hilo litokee, kama sijamuachisha shule na kumrudisha kijijini................yaani najuta kumleta mjini.......
 
ndivyo ilivyo; but wat i can say ni kwamba u have gud concept in ur mind over huyo bint lakini pamoja na yote 'DONT ACCEPT FAILURE NO MATTER HOW OFTEN IT VISITS YOU, NEVER GIV UP, NEVER'
 
Heshima yako baba,
Kiukweli hapo uko sahihi kbs kutilia ngumu hiyo posa,
Huyo binti angejifikiria tu kwann hyo bwana anataka kumuache mwanamke aliyezaa naye aje muoe yeye?
Km anaweza kumuacha huyo mwanamke atashindwa nn kumuacha yeye,
Sema ishu ya shule hapo nina wacwac km patasomeka!!!!!!
Nashauri mpeleken veta akapate ujuzi ajiajiri elimu ya kupambana darasan huyo hana dalili ya kusoma kbs.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…