Nimekatwa ppf, lakini mwajiri hajanipelekea

chaArusha

Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
88
Reaction score
31
Habari ndugu zangu. Naomba msaada wenu wa nini nifanye. Nimefanya kazi kampuni moja binafsi kwa miaka miwili, nilikuwa nikikatwa malipo ya PPF kwa muda wote huo hadi pale nilipoamua kuacha kazi.
Nilipokwenda katika ofisi za PPF kudai fedha zangu, nilipewa fomu ambayo ilitakiwa kujazwa na mwajiri, lakini nilipompelekea alikataa kujaza kwa madai kuwa hakuwa na fedha za kupeleka huko. Nilipokwenda PPF kuwaeleza hivyo, walinishauri niandike barua ya malalamiko ili wao waipeleke kwa mwajiri wangu.
Nahisi kama nimeibiwa na huyu mwajiri, alikuwa akinikata kila mwezi na hapeleki zinakotakiwa. Naomba kujua haki zangu ni zipi na vipi nitapata?
 
Kamshtaki PPF wao ndio watambana
 
Umeshaambiwa andika barua mbona hujafanya hivyo ...very good step to start with
 
Jaambo la kwanza kufanya ni kuandika hiyo barua maana huu ni wizi ambao umefanywa na mwajiri wako na uvunjaji wa sheria.
 
very simpo mfungulie kesi ya jinai onana na mwnasheria wa ppf kuna kifungu cha kuwashtaki waajiri kwa kesi ya jinai utaona kesho yake analipa akipandishwa ndinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…