Habari ndugu zangu. Naomba msaada wenu wa nini nifanye. Nimefanya kazi kampuni moja binafsi kwa miaka miwili, nilikuwa nikikatwa malipo ya PPF kwa muda wote huo hadi pale nilipoamua kuacha kazi.
Nilipokwenda katika ofisi za PPF kudai fedha zangu, nilipewa fomu ambayo ilitakiwa kujazwa na mwajiri, lakini nilipompelekea alikataa kujaza kwa madai kuwa hakuwa na fedha za kupeleka huko. Nilipokwenda PPF kuwaeleza hivyo, walinishauri niandike barua ya malalamiko ili wao waipeleke kwa mwajiri wangu.
Nahisi kama nimeibiwa na huyu mwajiri, alikuwa akinikata kila mwezi na hapeleki zinakotakiwa. Naomba kujua haki zangu ni zipi na vipi nitapata?