Nimekimbizwa na nyoka aina ya Koboko

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
2,567
Reaction score
416
Wakuu jana jioni nilipokua narejea home gafla nilikutana na nyoka Koboko kafura katikati ya njia uku kapanua kichwa kimekua kipana kama upawa.

Ghafla akanitokea nduki anakimbia mbaya mbovu uwezi amini tumezungushana mtaani zaidi ya masaa 2 ndio nikampoteza maboya na kurudi home
 
Mkuu ulikuwa unaigiza Ze Comedy na huyo nyoka au? Kumbuka koboko hajazoea mitaa, yeye ukaa porini tu na sehemu za vichaka pia huwa akimbizi watu kwa mapenzi. Yeye ukiingia kwenye anga zake atakufokea ila akibanwa ndipo atajaribu kukugonga kuokoa maisha yake na kukupa wewe onyo japo itakuwa bahati kwako kuishi na kusimulia maana sumu yake akikugonga tu si rahisi kuishi zaidi ya dakika 7 kama hujapata first aid. Huyo koboko wako alikuwa Joti au Masanja Mkandamizaji?
 

koboko unamjua wewe?....huwezi kumkimbia hata kwa dakika tano. acha porojo
 
Koboko / black mamba avimbishi kichwa. Pia koboko anaspeed kubwa na sumu kali. Anaweza kukugonga mara10 ktk sec10.

Kama kweli alikuwa koboko usingekuwepo leo hii. black mamba co nyoka wa kawaida/kibisa

Moja ya nyoka wenye hatari sana. Tanzania wapo wengi sehemu gani?
 

Koboko hapanui kichwa huyo ni cobra.....
 

Hahahaa mkuu umenivunja mbavu na hilo swali ulilomalizia
 

halafu alivyokuacha wewe akaniibukia na mimi ni bala kanikimbiza siku mbili mfulilizo hapumziki nikakimbilia kwenye daladala ndo akaniacha !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…