Nimekoma kutumia Airtel Money.

Lusaa

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2011
Posts
270
Reaction score
112
Jana jioni nikiwa mitaa ya Sinza nilikuwa natafuta sehemu ambapo ningeweza kuweka Airtel Money kwenye simu yangu ili nimtumie mtu, nilikuwa nataka kiasi kama cha laki 2 mbili. Nikaanza kuulizia kwenye maduka amabyo yalikuwa na vibao vinavyoonyesha kuwa ni wakala wa Airtel Money lakini cha ajabu kila duka/kibanda nilicho ulizia hawakuwa na Airtel Money, zaidi tu ya kunijibu kuwa Airtel Money haipatikani, wanatusumbua sana, hawatuletei, hatupati virtual money, nina virtual kidogo siwezi kukupa yote… na blah blah za hivyo. Nilizunguka zaidi ya maduka/vibanda 10 na sikuweza kufanikiwa ila duka la Mwisho nililofika pale Survey ndiyo walionikatisha tama kabisa, nakumbuka dada muuzaji alinijibu kuwa mimi ninayo laki 2 lakini siwezi kukupa yote kwa sababu wateja wegine watakaosa, labda nikuuzie elfu 50 tu! Nuilichoka na hiyo 50 sikuchukua, mimi nilifikiri raha ya mfanya biashara ni kuuza kumbe kuna wengine wana reserve huduma kwa wateja ambao hata hawajulikani watakuja saa ngapi?

Airtel kwa kweli mnakatisha tamaa na huduma yenu hii mbovu kabisa, kumbe mnajua haipatikani ndiyo maana mnatuchosha na matangazo yenu kuwa inapatikana bure, mmekimbilia kututangazia matangazo yasiyokuwa na maana badala ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwanza. Halafu na nyie wauzaji/wakala kwanini mnakubali kuweka matangazo ya huduma hiyo wakati mnajua haipatikani?

 
WalishindWa wakiwa na ZAP unadhani AIRTEL MONEY itaweza? VODA NA TIGO ndiyo mpaka vijijini.
 

Kizuri hujiuza kibaya hujitembeza. Hii nguvu ya matangazo yao inanipaga mashaka sana na authenticity ya service yao!
 
Njoo Mbeya unachukua kiasi chochote unachotaka.
 
Tar 8 walitutumia sms za kubadili password,nikabadili juzi nikanunua mpesa kama 250,000 kwa mara ya kwanza kutuma airtel money,nikawa namtumia jamaa yangu kama laki 2 hivi,cha kushangaza password ikawa tatizo attempts zote 6 zikafail wakalock simu nikaenda ofisini kwao wakasema utapigiwa simu mpaka sasa siku ya pili sijui hatima ya pesa yangu,

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hawa jamaa hata IS yao ya speed kuliko zote wanayoisfia ni Ushuzi mtupu. In fact it is the slowest one in the market. Sijui TCRA inafanya nini. This is Daylight Robbery!
 
Watu wanalalamikia flotation zao zinasumbua sana nadhani watajirekebisha.
 
pamoja na matatizo mengi waliyonayo hawa Airtel money lakini vyombo/taasisi ambazo zinahuzuka kuwapa license ya kuendesha bado wapo kimya tu maana Internet yao hamna chochote kabisa yaani unategemea 3G volume lkn hata 1G bado shida (TCRA wapo) kuhusu money kwani BoT wamesafiri? tunaomba wafanye kazi
 
Nzagamba Yapi ndugu yangu eti wakiblock inachukua wiki mbili kufungua account yako tena. Mimi sijawahi pata logic ya hii kitu.
mimi pia natumia airtel wiki mbili zilizopita nilikuwa nashughulikia airtel money account yangu jamani walinizungushaaa...mara ooh baada ya masaa 48 utatumiwa ujumbe..ooh baada ya masaa 48 password itarudi 1234 then utabadili..mara ohh account yako haina hela ndo maana tunashindwa kuaccelerate tatizo lako kwa IT..mara ohh nenda kasajili namba yako...kumbe namba ishasajiliwa maana nlikuwa naweza access ile menu after 150*60#.mara ohh umepiga maranyingi so usipige tena subiri 48 hrs itakuwa sawa..nikangoja three days nkajaribu holla...nikapiga ndo nikaambiwa two weeks ndo account yako itakuwa ok watanitumia message. Tarehe 14 ndo wiki mbili ziliisha leo 17 sioni msg sioni simu..na wala siwatafuti.
Nmenunua line yangu ya tigo napata sms za bure..net bure...dk 15, na tigo pesa....ol kwa sh. 450.
 
Last edited by a moderator:

Hapo kwenye red,ni tatizo kwa wafanya biashara wengi.Hii imenitokea several times.Bottom line,"umebugi meeeeeen"
 
Hiyo eateli mane ni balaa, nilituma shs.40,000 tu! kwenda Masasi nilijuta; mpokeaji alihangaika sana kuipata na mwisho aliipata kwa kulipa 5000 kwa mtoaji. Hawana loloteeeee !Wamebugi meeeeeen!
 
Bure ni ghali!
Si wanatangaza kwamba kutuma na kupokea pesa ni bure? Sasa faid wanapataje? Au ndo hayo mateso bila chuki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…