Jana jioni nikiwa mitaa ya Sinza nilikuwa natafuta sehemu ambapo ningeweza kuweka Airtel Money kwenye simu yangu ili nimtumie mtu, nilikuwa nataka kiasi kama cha laki 2 mbili. Nikaanza kuulizia kwenye maduka amabyo yalikuwa na vibao vinavyoonyesha kuwa ni wakala wa Airtel Money lakini cha ajabu kila duka/kibanda nilicho ulizia hawakuwa na Airtel Money, zaidi tu ya kunijibu kuwa Airtel Money haipatikani, wanatusumbua sana, hawatuletei, hatupati virtual money, nina virtual kidogo siwezi kukupa yote
na blah blah za hivyo. Nilizunguka zaidi ya maduka/vibanda 10 na sikuweza kufanikiwa ila duka la Mwisho nililofika pale Survey ndiyo walionikatisha tama kabisa, nakumbuka dada muuzaji alinijibu kuwa mimi ninayo laki 2 lakini siwezi kukupa yote kwa sababu wateja wegine watakaosa, labda nikuuzie elfu 50 tu! Nuilichoka na hiyo 50 sikuchukua, mimi nilifikiri raha ya mfanya biashara ni kuuza kumbe kuna wengine wana reserve huduma kwa wateja ambao hata hawajulikani watakuja saa ngapi?
Airtel kwa kweli mnakatisha tamaa na huduma yenu hii mbovu kabisa, kumbe mnajua haipatikani ndiyo maana mnatuchosha na matangazo yenu kuwa inapatikana bure, mmekimbilia kututangazia matangazo yasiyokuwa na maana badala ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwanza. Halafu na nyie wauzaji/wakala kwanini mnakubali kuweka matangazo ya huduma hiyo wakati mnajua haipatikani?