Nimekosa amani mwanangu anakohoa kifua kikavu na hapati nafuu

Nimekosa amani mwanangu anakohoa kifua kikavu na hapati nafuu

concordile 101

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2013
Posts
3,379
Reaction score
6,624
Ni siku kama ya tatu mwanagu wa mwaka mmoja anakohoa kikohozi kikavu na usiku anapata taabu ya kupumua.

Mimi ni mfauatiliaji wa thread ya Coronavirus humu, nimekosa raha kabisa na isitoshe niko mbali nao.

Yaani kila nikifuatilia habari ya wataliii Arusha natamani kulia kwa jinsi serikali ilivyoshindwa kuwa serious na hili jambo.

Haiwezekani pamoja na safari zote hizo za kuingia na kutoka China, Italy, Korea kusiwepo na hata raia mmoja aliyeambukizwa.

Nilikuwa nasikiliza mahojiono ya Mchina mmoja Marekani anasema China waathirika ni zaidi ya milioni na vifo ni vingi sana tofauti na inavyotangazwa.

Hivi ukweli pamoja na yote hayo hakuna hata Mchina mmoja aliyeingia kwetu akiwa ameadhirika toka December mwaka jana?

Tukizubaa hawa watu watatupoteza jamani.
Wizara ya Afya kuweni serious. Hiki kidudu kikianza kuonyesha makucha tutaisha, hakuna cha makonda wa Said au Mwajuma wote ni maji tu.
 
Bill Gates juzi kasema hapa, zaidi ya waafrika milioni kumi wanatarajiwa kufa mara tu huu ugonjwa utakapoleta makucha yake ndani ya bara letu, more than 10million Africans, tujiandae kuzikana.
 
concordile 101,
Fua mashuka kila wiki, Piga deki kila siku, Usipikie ndani ya chumba unacholala, Fungua madirisha wakati wakulala, Usipulizie dawa ya mbu/manukata mida ya kulala au ukiwa ndani unafanya kazi nyingine
 
Huku kwetu Kwamtogole ukijisikia una dalili za Homa, kupumua kwa shida na kifua kubana, kukohoa. Kuna namba unaipiga, wataalmu wameandaliwa kushughilika na swala hili. Usiende hospitali utazidi kuueneza.
 
concordile 101,
Poleka mtoto hospitali , zingatia usafi wa nguo za mtoto anazovaa na zile zinazotandikwa anapolala, ikiwezekana zote azitumie siku moja tu.

Asizirudie
 
Peleka mtoto hosptial achana na kutafuta wa kumpa lawama au wachina wamekutana na mwanao tu?
 
Siku tatu hujapeleka mtoto hospitali unalaumu kuingia kwa wachina
 
Bill Gates juzi kasema hapa, zaidi ya waafrika milioni kumi wanatarajiwa kufa mara tu huu ugonjwa utakapoleta makucha yake ndani ya bara letu, more than 10million Africans, tujiandae kuzikana.
Bill Gates ni tajiri number moja duniani na neno lake moja lina nguvu sana... Lakini naamini Bill Gates sio mkubwa kuliko Mungu... Mungu ataipigania Afrika, japo natambua kuona mataifa ya nje yakitamani sana kuona maneno ya Bill Gates yanatimia

Jr[emoji769]
 
Hizo ni projections tu mkuu, zinaweza kutimia au kutotimia. Ilà trust me, likiingia bongo na hizi daladala/mwendokasi zetu, tuombe heri.
 
Back
Top Bottom