Nimekosa amani mwanangu anakohoa kifua kikavu na hapati nafuu

Nimekosa amani mwanangu anakohoa kifua kikavu na hapati nafuu

Ni siku kama ya tatu mwanagu wa mwaka mmoja anakohoa kikohozi kikavu na usiku anapata taabu ya kupumua.

Mimi ni mfauatiliaji wa thread ya Coronavirus humu, nimekosa raha kabisa na isitoshe niko mbali nao.

Yaani kila nikifuatilia habari ya wataliii Arusha natamani kulia kwa jinsi serikali ilivyoshindwa kuwa serious na hili jambo.

Haiwezekani pamoja na safari zote hizo za kuingia na kutoka China, Italy, Korea kusiwepo na hata raia mmoja aliyeambukizwa.

Nilikuwa nasikiliza mahojiono ya Mchina mmoja Marekani anasema China waathirika ni zaidi ya milioni na vifo ni vingi sana tofauti na inavyotangazwa.

Hivi ukweli pamoja na yote hayo hakuna hata Mchina mmoja aliyeingia kwetu akiwa ameadhirika toka December mwaka jana?

Tukizubaa hawa watu watatupoteza jamani.
Wizara ya Afya kuweni serious. Hiki kidudu kikianza kuonyesha makucha tutaisha, hakuna cha makonda wa Said au Mwajuma wote ni maji tu.
Ķampime blood picture
Huenda ana infection kwenye damu,mara nyingi kwa watoto inawaletea kikohozi kikavu
Usiku ndio kinakereketa mnooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom