Nimekosea kutuma MPESA, je kuna msaada au basi!

Toa ushauri jinsi ya kuwashitaki maana kama kosa ni lako ulietuma kwa nini umshitaki aliepokea bila hata kuomba wala hamfahamiani?kosa litaitwaje?toa ushauri tafadhali!

Kosa litakuwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu!!

Kama wewe siyo mwizi kwa nini uchukue hela haraka haraka na usepe? Si ungeenda kuisalimisha!! Huyo ni mwizi tu lazima ashitakiwe akipatikana. Ila Mahakama zetu na Policcm sijui kama hii wataikubali.
 
Msaada ni mdogo na beneficiary ni mjanja hatumii tena namba yake kwa M-pesa
nasema hivyo kwani hata mimi nilikosea code namba kwa haraka na hizi touch screen zinataka umakini,nilipogundua nikawapigia Voda wakasema amechukua tayari ila watamblock..simu akawa amezima hadi siku ya pili akawasha tukaongea nae mwanzoni alikubali na kuonyesha ushirikiano but later akatuambia wazi harudishi na tufanye tutakalo.kwa kuwa nilipata jina lake(eliashea makundi) na pesa kachukulia moshi mjini nikajua nimeliwa babangu
lakini ni kukosekana kwa kanuni kali na uasilifu wa mtu na mti.binafsi nilitumiwa pesa kumbe ni ada ya mwanafunzi nilipowarejeshea wagosi wale hawakuamini wakanitumia na asante ya airtime lakini mimi niliwaambia si haki yangu hizo pesa na pia technology ipo wazi kiushahidi itaninasa nikikusudia vibaya na pia nikajiweka position yao kuwa hata mimi naweza kukosea

kukiwa na taratibu nzuri watu wasingekuwa wanakatalia pesa za watu..ni mfumo mbovu tu hamna ushirikiano wa makampuni ya simu na pia polisi kwa upande mwingine hawako wazi kwa hili
 

Sio kweli mkuu ,mimi ni wakala na ninatumia Voda jina linatokea baada ya kuwepa namba ya siri na kabla kuthibitisha!ukiona jina hakuna ujue mtu unaemtumia hajasajiliwa au umetuma nje mtandao wa Voda.
 

Mkuu kuna issue ipo kwa wadau wa sheria kw amuda mrefu sasa,vipi system ya bank ikikuwekea pesa kimakosa ghafla una salio x ukakuta salio y,ukasubiri hata miezi 6 hazijatolewa,(ukiwa wajua au kutojua) inategemea na transaction zako na umakini wako kwenye hiyo account....hapo ukizitumia au kuzitoa na kushitakiwa kama muhujumu uchumi...itakuwa ni haki kweli??
 
Lambardi. hivi benki ukitoa pesa sisizo zako huwa kuna utaratibu gani?
 
Last edited by a moderator:
Lambardi. hivi benki ukitoa pesa sisizo zako huwa kuna utaratibu gani?

Unashitakiwa kama mwizi mwingine, kama unaona salio limezidi toa taarifa kama ambavyo utalalamika salio lako likipotea. Suala la kukataa kurudisha hela zilizotumwa kimakosa na mhusika kuachwa huru ni uzembe wa mfumo wetu wa usalama, pili ni wizi wa wazi kama wizi mwingine. Tusiweke visingizio hapa. Ng`ombe wa jirani akiingia zizini kwangu anageukaje wangu?
 
kuna rafik yangu alitumiwa pesa kwa mpesa kimakosa kwenye simu yake million 1 jamaa alichofanya kutoa pesa fasta na akaichana line,sasa hiv ana line nyingine mpya yuko kwa mtaa

mwizi huyo!
 
Niliwahi kupewa namba iliyokosewa nikamtumia mtu tofauti, lakini nilipowasiliana na huduma kwa wateja waliweza kunirudishia ndani ya masaa 24
 
Next time ukikosea usihangaike kumpigia uliyemtumia, unapiga/unaenda ofisi za VODACOM watakurudishia hela yako ndani ya 24 hrs japo sometimes kuwapata huduma kwa wateja nako ni issue all the time wako bize
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…