Nimekosea wapi ndugu zangu msaada, nifanyaje?

Nimekosea wapi ndugu zangu msaada, nifanyaje?

Piscine

Member
Joined
Sep 28, 2014
Posts
36
Reaction score
10
Ushauri please,

Mimi na mpenzi wangu tupo kwenye mahusiano kwa miaka kama 2 sasa. Kwa zaidi ya mwaka nimekuwa na matatizo ya erection na kukosa hamu kabisa ya mapenzi.

Nashindwa kabisa kumaintain erection, nimekwenda hospital nimeambiwa testosterone imeshuka sana, nimepewa dawa lakini wapi mambo ni yale yale.

Natamani kuoa lakini kwajinsi hari yangu ilivyo namuonea huruma mtoto wa watu ataishi maisha gani na mimi kwenye hari hii. Huwa inatokea nashindwa kuperform sometime dudu ikisima hata dakika haichukui inalala msichana huwa ananicheka tuu! nimehama hadi nilipokuwa naishi iliniwe mbali nae lakini bado hunifuata.

Nilimkimbia ilikama anamtu apate nafasi ya kuwa nae, na azione tofauti zilizopo then atafanya maamuzi sahihi.Herbal clinic nimezunguka mpaka nimechoka, naona napoteza pesa zangu tu.Yani mapenzi kwangu imekuwa ya kuvizia tu.

Sasa jana kaniuliza unakuja lini kujitambulisha nyumbani?

Ikabidi ni mwambie kwanza kunajambo naomba tuonge, nikamwambia kuhusu hili tatito langu nijue anasemaje juu yahili? Majibu yake sasa,amekasirika anasema nimemuharibia maisha, kama nimepata mtu sinimwambie tu.amenitakia maisha mema pia anasema hata nitafuta tena tenaaa.Amekasirika hataki kupokea simu yangu wala kujibu text zangu.

Nimekosea wapi ndugu zangu? Nilitaka kuliweka sawa hili ndo mambo mengi yafuate sikuwa na maana mbaya kwasababu na mpenda kiukweli.Nasoma humu jinsi wanawake wanavyolalamika kwenye ndoa zao nilitaka kumuweka tayari kwa hilo.

Ushauri ndugu zangu nini chakufanya kumpenda nampenda sana tuu
 
Go three ways. Kwanza tatua tatizo kabla ya mahusiano. Waone madaktari bingwa wa afya ya uzazi. Wape muda. Ukiona hakuna suluhu wajaribu watu wa tiba lisha pia go spritual. Kwenye ukristo tunaamini kwenye maombi. Inaweza kuwa mapepo.mizimu.uchawi. usiende kwa mganga tafadhali.
 
Pole maana sikupatii picha
 
Kama yeye hajawahi sema ni tatizo wewe kiherehere cha nini? Pengine anarizika!
 
Mmmhmmh.. some women duh.. Lord help us and forgive our sins.. Naomba nikupe pole kwa unayopitia.. Binafsi sikushauri kukosa Amani na Furaha. If ulijaribu kupata tiba hospitals nakadhalika na ikashindikana still usife moyo . Naomba usifikirie kuoa kwanza for now ili tatizo lipate tiba then ndio uowe. Jaribu kupata msaada Wa kiroho Wa Maombi kwa maana kuna mambo mengine ni Evil Spirits. Sijajua kama ni mkristo or muislam but just elewa kwa Yesu haijalishi ni dini gani Bali ni imani yako ndio itakuponya..Huyo Dada anafikiria tuu ndoa ili aonekane na yeye ameolewa lakini akifika huko ndani ya ndoa sidhani kama ataiweza. Kama alikuwa na busara angekusikiliza tatizo lako pale ulipotaka kuongea nae na kukusupport 100% kwa Ku make sure hilo tatizo liko solved before hamjaoana . Nakushauri usiende kujitambulisha kwanza. Ni bora akulaumu now kuliko baadae after marriage. Kuna possibilities akaja shindwa kukuvumilia na kuanza kuku cheat na
Dharau on the top. Dear kama ni wako atarudi tuu usijipe pressure for now angalia suluhisho ya tatizo ulilo nalo kwanza. Thanks..
 
tibu kwanza hilo tatizo halafu baada ya hapo ndiyo uingie kwenye mahusiano serious .......kwa sabau wewe kisaokolojia pia umeshaanza kujiharibu kwa kujiambia kuwa hutaweza sasa wewe ukishaanza tiba we piga mademu ila wasiwe ndiyo wapenzi wa ukweli ukweli ukishajiridhisha sasa unaweza kupiga kazi tafuta demu wako wa maisha .. au uwe unatumia mkuyati
 
Kama yeye hajawahi sema ni tatizo wewe kiherehere cha nini? Pengine anarizika!

Dear I don't think so.. most of women are very secretive especially when it comes on marriage and sex .. wako radhi kwenda kucheat kuliko kusema hawaridhishwi .. So its better to talk first than to run in to marriage that will not last.. Thanks..
 
Pole sana mkuu. Tatizo ni kwamba hajapokea huo ukweli. Kwa mtazamo wangu anaona unamdanganya na unatafuta sababu ya kumwacha
 
Pole sana kamanda lakini Maelezo yako yanaonesha mpenzi wako huyo kuto tatizwa na hiyo hali kwa sasa, labda kwake mapenzi ni zaidi ya sex lakini pia machine kushindwa kufanya kazi kama inavyo takiwa ni tatizo kubwa sana kwa mwanaume hasa kisaikolojia.
Nakushauli utafute tiba ya hilo tatizo mapema kwani hutoweza ya furahia maisha. Hata ukiwa na pesa hilo tatizo litakufanya ujione maskini na kukosa raha daima.
Pia mzizimkavu anahusika sana hapa, akusaidie nini ufanye kutatua tatizo ila kwa Mimi na kushauri upate tiba ya kisaikolojia kwanza.

Pole sana kamanda na usimuoe huyo mpenzi wako mpaka utakapo tatua tatizo lako otherwise litajitokeza tatizo lingine la kugongewa nje.
 
ulifanya vizur kaka kumwambia.
usichoke kwenda hospitali, waone wataalam wa lishe, am a nutritionist also lkn pia kwa imani yako, mshirikishe sana Mungu kwenye hilo jambo kwa maana HAKUNA JAMBO ASILOLIWEZA. usijali
 
Umefanya uamuzi wa busara sana kutokukimbilia kuoa uko sahihi na hujafanya kosa, Anza upya kurudi kwa Madr. wa maswala ya uzazi na pia uwe muwazi kumueleza dr. mwenendo wa maisha yako, wakati unaendelea kwa dr. na maombi yaendelee na usinywe kila miti shamba unayoambiwa na kupewa, mengine huzidisha mabalaa, kuhusu huyo mwanamke kuna mambo 2 aidha hilo jambo alishaligundua na linamkera rohoni hataki kukwambia, na ulipomwambia alishkuru ili hapo hapo apate pakutokea yani kukuuacha, Na pia inawezekana ikawa kwake bado hajaona kama ni tatizo na anadhani labda unamdanganya cha kufanya endelea kutafuta tiba kama ni wako atarudi tu, ni bora usiingie kwenye ndoa kwanza mana utakuja kuumia mara 2 mpaka ukawaza kujiua pindi utakapogundua ana cheat na dharau anakufanyia kwahiyo utakuwa unalia na mambo zaidi ya 2. pole na kila kheri.
 
hilo tatizo linatibika as long as inasimama ila haichukuh muda basi tatizo ni hormones haziko balanced, ila dose yake ni ya muda maana huchukua takribani miezi mitatu, usijali utapona, ntaku-pm namba ya doctor wangu utamalizana naye mwenyewe, pole sana!
 
kuna kasi kubwa sana ya same sex male inaendelea hasa dar moshi na arusha,pls pombe kali,,in five years itakua shida,,
sijaelewa ni hii digit revolution au nini,,,,hasa vijana kutoka moshi ni shidaa..

play with saikologia yako pia zingatia balance diet na kwa sasa acha pombe.
 
Mungu amekuepusha na ndoa yenye mogogoro,huyo msichana mpotezwe tu. sasa mwombe akuponye na kukupatia mke atakayekufaa.
 
Mkuu kwani mpenzi wako ana umri gani? Perhaps she is just too young to comprehend seriousness of what you are facing? Or maybe yuko in denial ? Ila kama si mtoto then I'd say ni mnafiki na anasumbuliwa na tamaa ya ndoa.

Side note: Kudos to you for bringing the issue up vs. sweeping it under the rug. If I were on her shoes I would have been appreciative instead of kukasirika. We all know matatizo hayakimbiwi, sooner or later you they will catch up to you and then.......................
 
Go three ways. Kwanza tatua tatizo kabla ya mahusiano. Waone madaktari bingwa wa afya ya uzazi. Wape muda. Ukiona hakuna suluhu wajaribu watu wa tiba lisha pia go spritual. Kwenye ukristo tunaamini kwenye maombi. Inaweza kuwa mapepo.mizimu.uchawi. usiende kwa mganga tafadhali.
asante ndugu nitafanya kama hivyo, asante sana kwa ushauri wako.
 
Back
Top Bottom