Deejay nasmile
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 5,794
- 5,352
Yaan hapa nimechanganyikiwa hatari
Nilikuwa natoka natoka hapa mitaa ya mabibo hostel naelekea riverside.mbele kidogo nikaona kifungashio cheusi kando kidogo ya barabara kinaonesha kama kina kitu ndani.watu wanakipita tu, sasa sijui hawakukiona au ndo ubize tu wa mjini.
basi nilipokikaribia bila aibu nikaokota na kuendelea na safari mdogo nikitafuta sehem niangalie kuna nn...basi nikaingia kiduka flan kinauza uza vinywaji kuna ile miavuli ya jua nje..nikakaa nikachungulia ndani nikaona bahasha ya kaki ina nembo ya nmb na kadi ya bank (atm card).
Nikiwa na presha na hofu tele nikaichana ile bahasha ikiwa mule mule ndani ya kifungashio. Daaah!! Nakuta noti kibaoo za elfu 10 ..nikafunga fasta na kuinuka kuelekea upande wa pili kuna baa moja hivi..
nikaingia na kupitiliza moja kwa moja chooni nikajifungia huko na kuanza kuhesabu....ni pesa taslimi milion 9 zilikuwa mule..yaani nilipata kiwewe hatari kilichochanganyika na furaha na sala kama zote yaani.
Ghafla kuna mtu akagonga mlango ule wa chooni..kwa mshituko nikazifunga tena fresh na kutoka nje..ili niangalie utaratibu wa kurudi gheto nikaanze kupanga bajeti sasa.
Ghafla nikashtuka toka usingizini.kumbe nilikuwa nao ta tu ndugu zangu..sasa sijui hii ndoto ina maana gani wakuu...watalaam wa ndoto naombeni mnitafsirie ndoto hii!!