Poa sana, ila ukifika naomba uwape salamu zangu wana bendi pale klabu inayoitwa 'Whatsapp'. Waambie ni yule Mkenya aliyekua anacheza sana na kuagiza agiza nyimbo huku akiwanunulia beer, ambaye walikua wakitambua uwepo wake kwa kutangaza kwenye kipaza sauti.
Halafu kuna klabu nyingine inaitwa Oxygen, pale pia nilizikwenda chini kwa chini.
Sifa za mademu wa pale binafsi sikuona chochote tofauti nan kwengine, labda wanilizimia tu kisa sio wa huko. Tanzania ukitaka kunogewa kwa mambo ya mademu nenda Tanga, wale wana undugu na Mombasa hivyo wanakufanyia mambo utaishia kuisahau +254.
Yote tisa, Tabora patamu hali ya hewa ni kama ya Nairobi japo bila mbwembwe za kimjini. Chakula kitamu cha shambani, utadhani upo kijijini Nyeri au Uluhyani.
Kwa kweli niliona malori makubwa yamebeba ng'ombe japo sikufuatilia maana kazi iliyonipeleka huko ilinibana sana, lakini nategemea kurudi walau mara moja kila baada ya miezi miwili, pia nitashuka hadi pale Kigoma. Nina shughuli za kikazi Kaliua, Mpanda, Tabora, Mwanza na Isaka.