Nimekubali kuachwa tena

Nimekubali kuachwa tena

The Garang

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
2,880
Reaction score
4,830
Nianze kwa kucheka kwanza.

Hii stori naiandika kwa lugha isiyo Rasmi, lugha za kiujana ujana.

Wayback nlikuwa na mamiloo, alinipenda ye then mie nikausoma mchezo tukawa wapenzi. Tumeenda miezi kadhaa penzi likaanza kumiss, nikajaribu boost boost haikuwa ridhiki likafa Baada ya kukaushiana tu kila mtu akasepa na zake. Hii ni mwaka jana.

Mwaka huu mwanzoni wa mwezi Feb Binti akawa na shida na mie ndo ninaeweza kumsaidia, ilipigwa simu ya jamaa yangu na nlivopokea nkaisikia sauti yake, na kumtaja jina lake akabaki anashangaa nimejuaje kama ni yeye, but hivo naijua sauti yake na namna yake ya kuongea, akaeleza shida yake, nikamsaidia.

From that moment onwards, tukaanza wasiliana Tena kama zamani lakini sikuwa namzingatia sana maana ashasepa awali bila kuaga namie sikuwa bothered kuulizia nn shida.

This time kaja sikutaka muuliza what happened in our last relationship, anakuja na maswali ya kuniuliza indirectly kama nampenzi now namie jibu langu Niko single ili nijuee her next move. Kaja na bra braa kibaooo tu mie namsomea radar, penzi limeenda kiasi nikaanza ona red flags zisizoeleweka.

This girl is almost 3 years older than me so she is approaching her 30, Yuko desperate sana na mtoto but nyumbani anaogopa coz kwao ni familia flani hivi za dini dini sana.

Binti hayuko romantic kabisaa ,chatting zake ni boring hazikupi mood ya kuendelea kuchat nae, hanaga story sana BUT she is real a wife material kwa tabia zake, SHIDA inakuja Binti anaonekana anakaumimi au kauchoyo flani hivi as per mie na nlivolelewa naona hizo tabia siwezi endana naye

Mosi, hapendi kujihusisha na mambo ya kijamii, yeye anakasehem anaingiza Senti 5 sio haba, Kuna siku tunapiga story seriously ananambia ye hawezi hata siku Moja kuchangia sherehe yeyote Ile na sio kuwa hana Hela au laah hata akiwa nazo hatofanya hivo naye hataki sherehe yetu Ichangiwe na watu.

Duuúh nikaona hii Kali mie navopenda shughuli hivi ntaja mkwaza mtu au namwambia apeleke Hela ya mchango wa jambo fulan akapiga panga nije kumtia makofi Bure.

Pili, kuna siku nimemtext ... Hello my love kaja kunambiaa unajua mie dadako, nikaona huyu kaanza kutokuheshimu, nikamjibu ... So Then hakujibuu. Kakaa kimya we mie nikabidi nijishushe nikamtext umeshindajeee etc .

Tatu, nshasahauu mara ya mwisho nimeambiwa napendwa lini, ikumbukwe ye ndokanitaka namie kwa huruma zangu nikamfungulia lango Moja wazi la moyo ila akafikia tu seburen[emoji28][emoji28], on contrary mie ndo nimekuwa nagonganinsha sms za nakupenda, good night, good morning but she didn't respond na anaview status zangu nakupost shit zake. Leo kanipostia ... Vile unaenda kuomba msamaha alafu unakuta tayati Yuko kwa MAHUSIANO mapya.

Nne, ana ego ya kijinga kwake samahani ni ngumu kutamka I wonder if she becomes my wife huko nyumban itakuwaje au ni vile ananiona mdogo kwake.

Na kalivo kashenzi ukikaomba mchezo kanachekeaa tu au ndo hakajibu sms mazima utamkuta status kapost meme.. mwanamme tujjfunze kuwasaidia wapenzi wetu waafikie malengo Yao kuliko kudemand sex tu.

Nkakaona kajinga. Hajala hata 100 yangu, so at this point I have reached END OF THE ROAD. I have considered it as a Bad debts , not expecting to recover it.

Only those two failed attempts zimemtosha.

NIMEKUBALI KUACHWA.
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] nianze kwa kucheka kwanza.

Hii stori naiandika kwa lugha isiyo Rasmi, lugha za kiujana ujana.
Kubali aiseh huyo sio mwanamke tafuta unaemzidi umri....na akifikisha 31 kuolewa ndo asahau
 
Tusipotezeane muda,
uyu Mtoa mada Ni SUPER Marioo,

Ntatoa sababu zifuatazo

1. UNATABIA ZA KUPENDA MSELELEKO au GANDA LA NDIZI.
yaan Huwajibiki kabisa kwa mwanamke wako.
"....Nkakaona kajinga.
Hajala hata 100 yangu..."

Mtoa mada Unaishije na mwanamke hata Mia yako Hali, are you serious [emoji848]

2. UNA TABIA ZA UCHAWA CHAWA
yaani ni Kijana wa party after party afu Bill ikija uchangii,

[emoji117]"...navopenda shughuli hivi ntaja mkwaza mtu au namwambia apeleke Hela ya mchango wa jambo fulan akapiga panga nije kumtia makofi Bure....."

[emoji117]" utamkuta status kapost meme, mwanamme tujjfunze kuwasaidia wapenzi wetu waafikie malengo Yao kuliko kudemand sex tu ...."

3. UNA TABIA YA KUPENDA KULELEWA.
yaani Unadate na waliokuzidi umri na kipato, kwa kwasababu tu ili upate kukwepa gharama za maisha.

[emoji117]...This girl is almost 3 years older than me so she is approaching her 30.."

[emoji117]"....Binti anaonekana anakaumimi au kauchoyo flani hivi as per mie na nlivolelewa naona hizo tabia siwezi endana nae.."

[emoji117]"....yeye anakasehem anaingiza Senti 5 sio haba.."

4. UNA TABIA YA GUBU,
yaani unapenda kutoa excuse za kubumba kwa matatizo yako mwenyewe.

Mf 01: Kuna mahali unasema kinachomuweka na wewe kwny mahusiano Ni kuhitaji mtoto na ndoa na wewe, wkt ukichunguza mwanamke wako anahitaji usimame Kama mwanaume.

Mf 02: mwishoni unajisifia mwanamke hajawai kula hata Mia yako, ila Kuna mahali unalalamika mwanamke anakuchoyo na kaubinafsi. Wkt Katikati unatwambia yeye ndio huwa anaclear bills zote.

5.UNAPEMDA MAHUSIANO YA KUGANDANA KAMA WATOTO WA SEKONDARI.

[emoji117]".....on contrary mie ndo nimekuwa nagonganinsha sms za nakupenda, good night, good morning but she didn't respond..."

[emoji117]"....nshasahauu mara ya mwisho nimeambiwa napendwa lini..."

6. UNAPENDA KUPEWA UMUHIMU USIO KUA NAO

Mf 01: Umeomba mechi umekutana na status ya kijembe.
Ndio alikua sahii maana Unachojua ni kuomba mechi TU ila hata Ela ya sabuni hutaki kutoa, unategemea atakuheshimu vipi.

Mf02: Kuna mahali unalalamika kakuita mdogo wake.
Alikua sahii Sana maana anaishi na wewe Kama mtu na mdg wake, sio mtu na mwanaume wake.
Yaani huwajibiki Kama mwanaume, Ni tegemezi Kama madogo zake uko vijijini.

Mf 03: Kuna mahali unalalamika hakwambii anakupenda, hajibu sms zako.
Mwanamke Yuko sahii 100% , yaani aache kazi zinazomuingizia kipato ahangaike kujibu sms zako na kukwambia anakupenda kila Mara, kwa kipi Sasa cha muhimu unachoongeza kwenye maisha yake?[emoji848]

Kwa hizo fact 6 hapo juu,
Mtoa mada wewe Ni 100% pure MARIOO.
 
Hapo utapoteza mda na kuchezewa kihisia na huyo mswahili, hembu acha apite kama miaka iliyopita.

Sent from my itel P32 using JamiiForums mobile app
Kunichezea kihisia sio rahisi but ye ndo anajiharibia sababu tangu aondoke mara ya kwanza sikutaka Tena kumzingatia hii mara ya pili so alikuwa Kama geresha
 
Wewe sio mvuvi.Uvuvi unahitaji uvumilivu.Yaani wewe chambo imetikiswa tu unavuta ndoano.
Hata kuku anapewa mchele anakula anashiba halafu anadakwa analiwa na wali.
Wacha pupa.
 
Kunichezea kihisia sio rahisi but ye ndo anajiharibia sababu tangu aondoke mara ya kwanza sikutaka Tena kumzingatia hii mara ya pili so alikuwa Kama geresha
Sawa lakin huona hivyo vijembe status vinakunyima raha, ndo kuchezewa kihisia huko, mara umwambie i love u akuambie mimi dada ako, tena ukiomb sex, anacheka tu na kurusha jabali status [emoji23], ndo kuchezewa kihisia huko mkuu, futa namba mpotezee kiaina, hilo penzi halina tena vibe.

Sent from my itel P32 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom