Nimekuja Gundua kwanini watu wa Dar wavivu kupika, na kutegemea fast foods.

Huu mtazamo wako, unakinzana na uhalisia uliopo jijini Dar, ninacho kiona ni kuwa walio na majukumu makubwa ni watu wa mikoani lakini wao ndio wanapata mda wa kupika,

Nani anaye pata masaa 6 kupika?

Kwa vyakula wanavyokula watu wa Dar na pesa wanayopoteza per day mbona wangejipikia wange pata kula vizuri kuliko chips zege na kachori za kila siku?
 
Dar ina Kila aina ya watu, Dar watu wa aina zote utawakuta kule, ila wengi wanaotegemea fast food majority ni wale wanaofanya Kazi maofisini nk, hao wa vibarazani wengi wao hupika, tena ni wataalamu wa kupika mapishi mazuri, sema pia ukute hajapata pepo la vikundi vya kausha damu na marejesho maana linawamalizia pesa huko uswahilini mwisho wa siku unakuta mdada ameachiwa pesa ya chakula anachukua kiasi karibu chote kwenda marejesho mwisho wa siku kiepe kavu Cha buku jero na tomato nyingi ndo mtu anashindia
 
Umeongea kweli kausha damamu na heka heka zao za mrejesho pia huishia kula chips kavu... Kweli umaskini na tamaa ka kupata kwa pupa zinawaponza wanaishia kufutuka
 
H
Huu nao ni ugunduzi au ni nini?
 
Mbona dada zenu wa kanda ya ziwa wanakimbizana kutafuta nauli ya kuja Dsm.
Wanakosa nini kwa wanaume wa Bara?
Hawa kimbiliii wanaume wa Dar, wanakimbillia mafanikio feki ya kudanganywa kideoni
 
Na hiyo ni moja ya element ya Urbanization.
Urbanization ndo ikufanye ukose muda wa kupika? Sawa unaweza kwa nchi zilizo endelea huku chakula kinavyoandaliwa tu, Ukisema ule hivyo daily kuugua ni kugusa tu
 
Kwa nini wanaume wa bara wanashindwa kuwadhibiti wanawake zao wasidanganyike na mambo ya Dsm
Are they too weak to that?
Ulimbukeni hautolewi kwa kuambiwa mpaka mtu akae prince kwanza ndo akili imkae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…