Ifahamike suala la mtu kuchukia mtoto wa mwingine ni la asili maana hata wanyama wengi wapo hivyo.Kinachomsaidia binadamu ni utashi tu. Hivyo, haishangazi mama wa kambo kuonekana hivyo.Hata mababa wengi tu huchukia watoto wa kambo,sema wanaume kwa kulinganisha ni wavumilivu, pia wao hawapo karibu na watoto.Aidha, ndiyo maana kuna kundi kubwa la wanaume hukwepa kuoa mwanamke mwenye watoto, baadhi ya sababu zikiwa eti mtu kashachakazwa na kuwa hawezi kulea watoto wa mwenzake.
Lakini kuna suala ambalo wengi tunakosea, kufikiri mtu akiwa mama wa kambo tu basi ni mbaya. Wakati mwingine wanajamii ndiyo hukuza suala hili. Wasione au kusikia mtoto ameadhibiwa, watasema. Adhabu ileile ambayo angeitoa mama mzazi,akiitoa mama wa kambo ni vita.Mimi nimelelewa na mama wa kambo, lakini si kila jambo baya analokufanyia au kukuudhi anafanya kwakuwa si mwanae, niliona maudhi mengi ni yaleyale anawafanyia wanae kila mtu kwa muda tofauti. Sasa mimi au ndugu zangu tusipokuwa wavumilivu ndipo tunakurupuka na kuanza kuwaka, huyu mama ni binadamu,nae anawaka, awapigie mogoti nyinyi ni nani?
Laiti wanajamii na watoto wangekuzwa kwa kutomuona mama wa kambo ni adui, tatizo lingepungua.Kumaliza haiwezekani, maana ni nature.Hivyo,ninakiri kuishi na wamama wa kambo kuna changamoto,lakini pia huchagizwa na wanajamii. Hii ni sawa na mtu na mawifi au mama mkwe.Maudhi yaleyale ambayo mama mzazi hukufanyia, akifanya mama mkwe anakunyanyasa.Na mkwe ni hivyohivyo,kosa lilelile analokufanyia binti yako wa kuzaa akifanya mkwe, hafai.