Katika MwanaJF ambae natamani nione nyuzi zake tena ni ndugu ONTARIO. Huyu jamaa nyuzi zake ukizipitia kuna kitu unapata umri wake, uthubutu wake katika kutafuta, kama unapenda maendeleo utahamasika.
Uzi nilioupenda zaidi ni yale mahojiano aliyofanya na Daby alishusha nondo za kutosha kuhusu uthubutu na umuhimu wa kutafuta taarifa sahihi katika ujasiriamali na biashara kwa ujumla. Alikua anachangamsha lile jukwaa Biashara, Uchumi na Ujasiriamali. Siku hizi limepoa hakuna nyuzi ambazo zinaweza leta fukuto JF.