Nakumbuka nilipokuwa O-level tulikuwa na mchezo wa kutoa majina ya utani kwa walimu,kuna mwalimu mmoja alikuwa na nyusi nyingi karibu zinaungana tukawa tunamwitw MANYUSI na mwingine aliingia class siku ya kwanza amevaa suruali ina mifuko miwili nyuma tukaanza kumwita DABO POKETI,mwingine alikuwa na Garden Luv la kitosha linachomoza hadi shingoni tukawa tunamwita MWAKIPESILE kwa kuwa tu kuna gazeti fulani lilikuwa linatoa katuni ya jamaa mwenye jina hilo aliyekuwa na garden kama ufagio.
Primary napo nakumbuka niliwahi kucheza kamari nikaliwa hadi nauli ya daladala ikatokea lifti nikaikimbilia na kusahau begi la shule,kesho yake nikakuta madaftari tu tena yamechanwa begi likaenda, begi lenyewe lilikuwa ni la mgongoni limeangikwa OASIS.