Nimekuta mtu anatumia makaa ya mawe kama mbadala wa mkaa

Nimekuta mtu anatumia makaa ya mawe kama mbadala wa mkaa

Mshuza2

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
11,261
Reaction score
17,202
Ikoje hii kiafya? Kwanza una harufu kali sana..ni kujiongeza baada ya gharama za gesi kupanda au tuiteje?
Ningependa kujua kama ni sawa au sio sahihi kwa matumizi ya nyumbani.
 
Yakiwa yenyewe haiwezekani kwa sababu yana moto mkali sana,sefuria hizi za mabati zinatoboka,Ila unawezwa kutengenezwa kwa ajili ya kupikia nyumbani kwa hizi sefuria za bati
 
yanafanya kazi fresh tu...unachukua mkaa wa kawaida ukiwaka unamix na vipande vichache vya makaa ya mawe...aisee moto hauishi
Ila yana harufu kali sana
 
Wazo langu ni kuja kujenga nyumba yenye fireplace na kutumia makaa ya mawe kama source ya joto. Je nitakuwa nakosea? Kiafya je ikoje?
 
Wazo langu ni kuja kujenga nyumba yenye fireplace na kutumia makaa ya mawe kama source ya joto. Je nitakuwa nakosea? Kiafya je ikoje?
yana moshi mwingi wenye harufu, ni kama umechoma tairi la gari,labda mpaka yawe processed kwa kupunguzwa carbon
 
Wazo langu ni kuja kujenga nyumba yenye fireplace na kutumia makaa ya mawe kama source ya joto. Je nitakuwa nakosea? Kiafya je ikoje?
Wataalamu wameshaanza kukueleza yanatoa kaboni monoksaidi kwa wingi, sasa hiyo fireplace utakuwa unaicha ikiwaka au unauzima? Utakuwa unauzimaje, na maji au utakuwa unafunga kuunyima oksijeni?
 
Ni nishati ya uhakika ila kabla ya kuitumia unatakiwa kutengeneza miundombinu ya kuondoa hewa ya ukaa kwa kujenga jiko mahsusi kwa matumizi ya kawaida. Moto wake hudumu kwa masaa 6-8.
Matumizi ya makaa ya mawe majumbani yanahitaji uwekezaji wa kutosha,kwa kuwa gharama ni kubwa, jambo hili linapaswa kufanywa na Serikali, kwa kujenga kinu kitakacho badilisha joto la makaa ya mawe kuzalisha umeme utokanao na mvuke.
Umeme unaopatikana ndio utumike majumbani.
 
Back
Top Bottom