Nimekutana na aliyewahi kuwa boss wangu katika interview za shirika la umma

goroko77

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
8,845
Reaction score
13,072
Wakuu habari za mchana

Leo nimekumbuka kisa kimoja hivi wakati wa kutafuta ajira za Serikali ilikuwa mwaka 2019 pale Tanga mjini katika interview za TANESCO Kanda ya Kaskazini .

Mimi niliweza kufaulu mtihani wa written ila boss wangu alifeli vibaya sana ule mtihani na kupelekea yeye kushindwa kwenda kwa hatua zinazofata ya oral.

Boss wangu yule ndie aliyenifanyia figusu kazini hadi kuondolewa kazini, ilikuwa ni kampuni kubwa ya mikopo kipindi hicho 2012.

Aliweza kutumia ugeni wangu ktk Kazi kwa kujichukulia mikopo kiujanjajanja na kupelekea watu wengi kufukuzwa kazi na yeye kuendelea kuwepo.

Nilivyomuonesha namba yangu ya mtihani alishanga sana kwa alama nilizozipata ktk mtihani ule ambao yeye alishindwa kufika hata c, akaniomba nimpe review ya maswal ili akiitwa tena awe amejipanga.

Maisha ni mzunguko sijui aliko ila nasikiaga ana bahati na kazi sana.
 
Kwa jinsi ya uandishi wako huu, unataka kutuamisha kwamba ulifaulu kweli?
 
Haki vile nilifahulu ..babu mtalamu wa hesabu na engineer wapi na wapi miandiko. Babu
Engineer kumbe na wewe ulikuwepo Tanga kwenye zile interview?

Aisee kulikuwa na nyomi sana wengine tuliitwa kwenye interview tarehe 21 tukaja kufanya interview tarehe 25. Tuliteseka sana pale Tanga ni kushinda kwenye kile ki bustani pale nje ya Tanesco.

Sikutoboa pia ile interview.
 
Natangaza mimi ni kilaza, nimekosa mimi, kama mtaweza wanaJF nisaidieni kuelewa.

Natanguliza shukrani zangu zangu za dhati kwenu.

Ahsanteni!
 
Boss wangu Yule ndie aliyenifanyiaa figusu kazin had kuondolewa kazini .ilikuwa Ni kampuni kubwa ya mikopo kipind hcho 2012 aliweza kutumia ugeni wangu ktk Kaz kwa kujichukulia mikopo kiujanjajanja na kupelekea watu wengi kufukuzwa Kaz na yey kuendelea kuepo
 
kama hata mwandiko wa @goroko Anafaulu kwenye interview nyie ambao huwa mnafeli huwa inakuaje kuaje
Babu kukosea kutype tu bas imekuwa hatuna akili .kak so wote walisoma hkl na hgk hgl hapan babu heshimu tahaluma zingine ambazo hazitaki blah blah
Au Ni wew umefeli written ile ??
 
Umeacha kulima au unataka kuacha kulima?
 
It's good kama haukumuonesha kinyongo na kumsaidia alipohitaji msaada kwenye hiyo interview..maisha ni mzunguko ipo siku atakushika mkono tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…