Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Leo asubuhi nimekutana na kitu cha ajabu. Mpaka sasa mwili unasisimka!Tofauti na binadamu wa kawaida yeye macho yake yako kifuani na siyo mawili bali manne!Ukweli miguu sikuiona ila kichwa kilikuwepo na hata mikono!Kadri nilivyozidi kumsogelea nilikuwa nikipigwa na upepo mithili ya beach.
Ilifika hatua uzalendo ukanishinda na kutimua mbio mpaka nilipofika barabara kuu ambapo nashukuru magari yalikuwa yakipita.Ajabu alikuwa kavaa nguo ambayo hadi sasa nimeshindwa kujua ni rangi gani maana ilikuwa ikibadilika.Macho niliweza kuyaona kwasababu mboni zilikuwa za kijani kali.
I say, ulikutana na mimi nikashangaa sana ulivyonikimbia! Hata mie nilikuwa nawasimulia wenzangu kwamba nimekutana na binadamu sijui kwa nini kaniogopa akanikimbia kama kaingiliwa kidogo agongwe na gari!
Tuonane tena kesho basi, pita njia ile ile saa zile zile tufahamiane vizuri!