Django Doer
JF-Expert Member
- Jun 30, 2023
- 2,865
- 5,184
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NdioOyaaa kwani kutumia jf ni Siri ??
Lakini pia inawezekana anatumia huu mtandao kwa kusoma tu taarifa na si member wa JF.Wakuu za usiku .
Leo baada ya kutoka kwenye mihangaiko yangu nikaamua kupanda daladala za kwenda Makumbusho.
Sasa siti zilikuwa zimeisha nikaamua kusimama tu, cha kushangaza aliyekuwa amekaa kwenye siti alikuwa anatazama JF😅 nilishtuka na kufurahi pamoja na kushangaa sana 🤣.
Maana kwangu mimi JF ni kama sehemu zangu za siri, hakuna rafiki au ndugu anayenijua kuwa niko humu.
Hata nikitumiaga JF naitumiaga gizani au sehemu isiyokuwa na watu.
Sasa we mama uliyekuwa unakunywa juisi ya miwa na biskuti nakushauri tu ujifunze kujisitiri ndio maana tunatumia fake IDs humu.
Si vyema ukatumia huu mtandao mbele za watu maana huwezi jua nyampara ni nani 💂💂💂🧑✈️.
Yangu ni hayo tu wakuu.