Nimekutana na mtu aliyeishinda Saratani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nilikuwa ninatembea kama sehemu ya mazoezi ya asubuhi, nilikutana na mama mmoja umri waka utakuwa 50+. Tulisalimiana na alinieleza kuwa haamini kuwa ametembea mwendo wa mrefu vile. Aliniekeza kuwa miezi sita iliyopita hakuweza mwendo ule kwani ndiyo alikuwa anamalizia vita na cancer.

Kwa kweli nilikuwa ninahamu ya kusikiliza zaidi kwani wengi ninaokutana nao katika vita hii hakuna niliyekutana nae baada ya vita. Wengi hawafikii kutoa ushuhuda, lakini kwa mara ya kwanza nimekutana na mtu aliyepewa all clear “touch the wood”.

Nilimuomba mama huyu anieleze zaidi. Aliniambia alihisi uvimbe kwenye ziwa. Haraka waliwahi hospitali na alifanyiwa biopsy. Majibu yalithibitisha malignant.

Alifanyiwa upasuaji na ziwa lake kutolewa. Aliwekewa ziwa la plastic. Safari ya chemotherapy ilianza. Ilikuwa ni kila baada ya wiki tatu mwanzo wa matibabu baadae ilikuwa kila baada ya wiki tano.

Alisema chemo ni sumu halisi. Baada ya session mwili unabaki na nguvu ya kupumua tu, pale unapoanza kupata nafuu ni muda wa doze nyingine.

Ana watoto wanne binti mmoja na wakiume watatu. Binti ameolewa na ana watoto wadogo. Wa kiume mmoja alishahama nyumbani. Lakini habari zilipowafikia yule wa kiume aliyehama alirudi na alisaidiana na wadogo zake pamoja na baba yao kuuguza.

Hospitali walipeana zamu kumpeleka na watoto wote walijifunza kupika. Kabla ya hapo mama ndiye alikuwa mpishi mkuu wa familia.
Mwisho alisema safari hii imemfanya amjue Mungu na kuwa karibu nae sana. Yuko tayari kuongea na wagonjwa na wa cancer na kuwaeleza kuwa ni safari ndefu na ngumu lakini kuna matumaini siku hizi.

Ninakumbuka zamani kidogo nilikuwa kwenye clinic na daktari bingwa aliyetoa majibu ya biopsy kwa wagonjwa. Baba mmoja alifika na mkewe na walipopokea majibu mke alianza kulia. Yule baba aliitikia tu sawa, nilipojua kuwa yule mgonjwa hakuwa pale kimawazo na itamchukua muda kuelewa ni pale mke alipoulizia safari ya matibabu.

Ni muhimu kuambatana na mtu unaemuamini siju ya kuchukua majibu.
 
Imani za kishirikina pia huchelewesha matibabu. Cancer ikiwahiwa na matibabu yakiwa mazuri unapona.
 
Some people pass through a lot of difficulties in their life. Na hasa udhaifu wa mwili. The good thing is, wengj humrudia Mungu na kuwa na amani.

Sent using Jamii Forums mobile app
There is a beautiful healing prayer I came across, it says “Lord you created me from nothing and as I belong to you, you can recreate me again without any illness if it’s your will”.
 
Imani za kishirikina pia huchelewesha matibabu. Cancer ikiwahiwa na matibabu yakiwa mazuri unapona.
I agree. Lakini pia dawa za kienyeji zinafanya kazi.

Mama yangu alikuwa diagonised na cervical cancer. Kuna mtu akamwambia aende kwa baba mmoja hivi akapate matibabu. Huyo baba amesajiliwa kabisa na wizara ya afya. Nilimwambia mama hayo ni mambo ya kiganga achana nayo, nikamuomba tuzidishe maombi.

Mama alinijibu kujaribu sio mbaya. Hapa ninapozungumza mama yupo cancer free. Baada ya yale matibabu, vipimo vilionyesha hana cancer.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Woh that is amazing Glory be to the God Almighty
 
There is a beautiful healing prayer I came across, it says “Lord you created me from nothing and as I belong to you, you can recreate me again with any illness if it’s your will.
The words are so perfect. Na zaidi, biblia inasema roho mtakatifu hutusaidia kuomba kwa kuugua kusipoweza kuelezeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
natamani uandike tena yaani iendelee kunaonekana kama kuna kitu imekikata kutokana na sisi wasomaji kutopenda kusoma habari ndefu! nimepata kitu ila si kwa kadri nilivyozoea kwa uandishi wako halafu mbaya sijui nakosa nini?
 
Km kila mtu humu atanena kwa lugha yake ya kitaaluma, nadhani jukwaani hapatakalika. Tukija na lugha zetu za C++, n.k mmmhhh
 
Mama yangu (RIP) kapigana na cancer for 14yrs. She put a hell of a fight and I'm proud of her kwa sababu through those 14 years, alifanikisha mambo mengi maishani mwake, and she went with a bang!

Kuna watu wameishinda kansa na wapo hai, ila vilevile kuna watu waliopigana hadi kufa na kansa mpaka wanakuwa ni motivation kwa vizazi vyao na jamii. Kupima na kujitahidi kuishi healthy, kunasaidia.
 
Tatizo lililopo kwetu ni kwamba inapo fik bahati tunaambiwa twende tukapime bure hatuendi man tunaamini sie wote ni wazima kumbe hata tunatembea tukiwa marehemu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIP mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…